OR-TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari. Majina ya Walimu haya yanatokana na Tangazo la Serikali la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na Walimu katika Shule za Msingi na Sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi mapema mwaka huu na hivyo kuondolewa kwenye Utumishi wa Umma.
Baada ya uhakiki wa maombi ya Walimu yaliyotumwa Serikalini, jumla ya Walimu 3,033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi. Kati yao, Walimu 266 ni wa Sekondari na Walimu 2,767 ni shule za msingi. Walimu hao watatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na kisha watakwenda kuripoti kwenye Shule hizo. Walimu hao wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 27 Desemba, 2017 hadi tarehe 07 Januari, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:-
(i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita;
(ii) Cheti halisi cha kitaalamu cha kuhitimu mafunzo ya Ualimu kwa ngazi husika; na
(iii) Cheti cha kuzaliwa.
Aidha, OR-TAMISEMI inawaelekeza walimu waajiriwa wapya waliopangiwa vituo vya kazi kuwa:
i. Vituo vyao vya kazi ni Shule za Msingi kwa walimu waliopangiwa kufundisha Elimu ya Msingi na Shule za Sekondari kwa walimu waliopangiwa kufundisha Elimu ya Sekondari na sio Makao Makuu ya Halmashauri.
ii. Mwalimu yeyote atakayebainika kuchukua posho ya kujikimu na baadaye kuondoka/kutoroka kwenye kituo chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
iii. Kila mwalimu amepangiwa kwenye shule ambayo ama haina walimu wa somo husika kabisa au kuna upungufu mkubwa shuleni hapo. Hivyo, waajiriwa wapya hawatahamishwa kutoka shule moja kwenda shule nyingine ndani au nje ya Halmashauri au Mkoa bila ridhaa ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
ORODHA YA WALIMU WA ASTASHAHADA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI KATIKA SHULE ZA MSINGI.pdf
ORODHA YA WALIMU WA SHAHADA NA STASHAHADA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI.pdf
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.