Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekamilisha zoezi la uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi vya Serikali kwa mwaka 2017 ambao walihitimu Kidato cha Nne mwaka 2016.
Jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775 sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9 walifanya mtihani wa kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2016. Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo mwaka 2016 walikuwa 47,751 wakiwemo wasichana 24,587 sawa na asilimia 51.5 na wavulana 23,164 sawa na asilimia 48.5.Watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Hivyo ufaulu katika mwaka 2016 uliongezeka kwa asilimia 3.15 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2015.
Bofya hapo chini Kujua Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017:
Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Kwanza 2017
Watakaochaguliwa Kujiunga Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi awamu ya Pili 2017
Aidha, fomu za kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (joining instructions) zinapatikana kwenye shule alikopangiwa mwanafunzi na kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.