Katibu Tawala Mkoa wa Pwai Rashid Mchatta amewaelekeza watumishi wote katika taasisi za umma mkoani humo kuhakikisha kuwa wanaainisha majukumu yao ya kazi kupitia mfumo wa PEPMIS kabla ya kufungwa Januari 24, 2024.
Ametoa rai hiyo leo Januari 16, 2024 wakati wa utiaji saini wa Mkataba wa utendaji kazi katika taasisi za umma kati yake na Wakurugenzi wa halmashuri za Mkoani humo na akawaasa Wakurugenzi hao na Wakuu wa idara za halmashauri kuwasimamia kwa karibu zaidi wasaidizi wao katika kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa wakati.
Amewasisitiza Watumishi hao kuwa makini katika kuainisha majukumu ambayo yataweza kutekelezeka na kupimika kupiti mfumo wa PEPMIS ambao ndio utakaotumika kupimia utendaji kazi zao.
“Heshima yako kama Mtumishi wa umma ni utendaji wako wa kazi katika eneo lako, hivyo mnapasawa kujituma ili kuweza kulinda heshima yako,” ameeleza Mchatta.
Aidha, Mchatta ameahidi kuwa atausimamia vyema mfumo huo na kuhakikisha utekelezaji wake unaenda kulingana na malengo yaliyowekwa.
Nae kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt Editha Rwiza amesea zoezi la kujengea uwezo Taasisi za umma Kupitia mifumo ya PEPMIS/PIPMIS lilianza rasmi tarehe 20 Novemba, 2023 nchi nzima.
Dkt Ngaiza alifafanua kuwa zoezi hili ilihusiaha mifumo miwili ni PEPMIS/PIPMIS na HR Assesment ambapo mifumo yote ilifindishwa kwa pamoja
Alieleza zaid kuwa kwa upande wa HR Assesment, zoezi hili lilikuwa limiwahusu wawakilishi wa Idara na Vitengo ili kuangalia mahitaji halisi ya watumishi.
Na mfumo Wa PEPMIS/PIPMIS unamuhusu mtumishi moja kwa moja hivyo bado zoezi la kutoa mafunzo linaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.