• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Aweso awataka Wakurugenzi wa mabonde ya Mto Kuhakikisha wanasimamia na kushirikiana na Watendaji wa Ngazi nyingine kudhibiti Uharibifu wa Vyanzo vya Maji

Posted on: November 7th, 2022

Aweso awataka wakurugenzi wa mabonde ya Mito kuhakikisha wanasimamia na ha kushirikiana na watendaji wa ngazi nyingine kudgibiti Uharibifu wa vyanzo vya maji .

Waziri wa maji Jumaa Aweso, amewaagiza wakurugenzi wa mabonde ya mito kuhakikisha wanasimamia na kushirikiana na watendaji wa ngazi nyingine kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji ili mito iendelee kubaki salama .

Aidha amesema changamoto ya upungufu wa maji ni kipindi cha mpito hivyo kila mmoja kwa nafasi yake kuanzia ngazi ya jamii washirikiane kupambana na tatizo hilo ili kurejesha hali ya kawaida ya upatikanaji wa maji.

Akizungumza na wadau wa maji mkoani Pwani, katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Pwani  ,Aweso alieleza Taasisi yoyote imara inapimwa kwa kipindi cha matatizo hivyo hakuna namna ya pekee ya kushinda vita hii zaidi ya kukubali ushirikiano.

"Nchi yetu ina mabonde tisa ,Wizara ya maji Ina wajibu wa kuyasimamia ,nimefanya ziara nchi nzima ,nimejifunza kuna mkurugenzi wa bonde ukimuuliza je anajua Raslimali za maji na mito lakini unakuta hazijui" Ni wajibu wetu kushirikiana pamoja watu wa bonde,TFS , watendaji wa maji, Mazingira kupata suluhu "

Hata hivyo Aweso alieleza ,maji ni muhimu ,na huduma ya maji haina mbadala ambapo kwa mujibu wa sensa Watanzania wapo milioni zaidi ya 61,ukikadiria mtanzania mmoja anatumia mita za ujazo wa maji 2,250 kwa mwaka wakati mwaka 1961 mtanzania mmoja alitumia mita za ujazo 12,000.

"Mwaka 1961 kulikuwa na takriban Watanzania milioni 10, maji ujazo wa milioni 126, kati yake Raslimali za maji zilizopatikana juu ya ardhi ilikuwa milioni 105 huku Raslimali za maji zilizopatikana chini ya ardhi ni mita za ujazo milioni 121, ukikadiria kwa mtanzania mmoja alikuwa anatumia ujazo 12,000 kwa mwaka."alibainisha Aweso.

Awali mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya na kamati za ulinzi kuhakikisha wanazuia kuchepusha maji na kuzuia uharibifu wa mito inayopita kwenye Maeneo yao.

Agizo jingine  kuhakikisha mifugo inayotoka mikoa mingine haiingi mkoa wa Pwani na iliyoingia irudi ilipotoka.

Kunenge alielezea kwamba , wafugaji wasitumie nguvu kudhuru wananchi,kwani hakuna alie na nguvu zaidi ya mwingine na atakaejaribu kufanya hivyo atashughulikiwa .

Aliwataka wafugaji na wakulima kuheshimiana ili kujiepusha na migogoro isiyo ya Lazima baina Yao.

"Mabonde ya mito,vyanzo vya maji yasimamiwe ,,wanaochepusha maji waache ili iwe salama "alisema Kunenge.

Akizungumzia changamoto ya uharibifu wa mazingira, Kunenge alikemea ukataji miti ovyo sanjali na uchomaji mkaa holela.

"Niliona picha ya dereva wa bodaboda akiwa amebeba magunia ya mkaa ,nikajiuliza hili wenzangu hamlionii ,hatushtuki hadi tupewe maagizo,"naomba tusimamie hili kupunguza tatizo la ukataji miti ovyo"alieleza Kunenge.

Mkuu huyo wa mkoa ,alieleza upo mkakati wa upandaji miti na kuangalia njia mbadala ya matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza tatizo hilo.

Mwenyekiti wa bodi ya DAWASA Jenerali mstaafu Davis Mwamnyange alisema ,maji ndio tegemeo kubwa kwa binadamu, na maji hayana mbadala ,lazima vyanzo vya maji vitunzwe ili DAWASA iweze kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha huduma ya maji inapatikana.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri,alieleza changamoto kubwa iliyopo Mkoani Pwani ni makundi ya mifugo inayoingia kiholela.

Alisema wapo wenye mifugo ambao wanailaza mifugo mchana ikifika usiku wanaitoa kuingia katika maeneo ya watu kulisha suala ambalo linakatisha tamaa juhudi za Serikali.

Msafiri kwasasa wamejipanga kuanza operesheni za usiku kudhibiti wanaoswaga mifugo nyakati za usiku.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.