Balonziwa Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda amepokea kwa mara ya kwanza shehena ya mananasi yaliyokaushwa kutoka Bagamoyo mkoani Pwani, kupitia kampuni ya Japani inafahamika kwa jina la Taishin Co Ltd.
Mapokezi hayo yamefanyika Septemba 24,2024 katika Bandari ya Tokyo, kwenye hifadhi za bandari hiyo za Kawanishi (Kawanishi Warehouse) jijini Tokyo.
Imeelezwa kuwa Shehena hiyo imewasili nchini Japan kwa ajili ya kutambulishwa katika soko la Japan, ambapo inatarajiwa kuanza kuuzwa kwenye maduka makubwa ya TOMIZAWA na LIFE CORPORATION yaliyosambaa kote nchini Japan.
Kampuni ya Taishin Co. Ltd ya Japan inashirikiana na Kampuni ya Elven Agri kutoka Tanzania katika kufanikisha kuleta zao hilo nchini Japan.
Imenainikuwa kuwa hii fursa kubwa kwa wakulima wa mananasi nchini Tanzania kufikia soko la kimataifa la Japan.
Ubalozi wa Tanzania nchini Japan umetoa shukrani kwa kampuni hizo kwa ushirikiano wao na jitihada walizoweka katika kufanikisha hatua hii muhimu, inayotarajiwa kuinua sekta ya kilimo nchini Tanzania na kuleta manufaa kwa wakulima wa zao hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.