Serikali imewahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze ,Mkoani Pwani kuwa wataondokana na tatizo la maji na kubaki historia ifikapo mwezi april mwakani.
Tatizo la maji limekuwa likiwapa shida wananchi hao kwa miaka mingi hali iliyokuwa ikiondoa imani na serikali yao.
Akiwahutubia Wananchina wa Chalinze, Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alisema kuwa ,shida ya maji Chalinze imekuwa kubwa ambapo wamekuwa wakikosa huduma hiyo ya maji safi na salama ya uhakika kwa kipinndi kirefu.
“Tukiahidi tunatekeleza, na serikali mkiiona haitekelezi baadhi ya mambo kwa haraka lazima inasababu na inatolea ufafanuzi wa kusuasua kwa jambo husika “
“Faraja inakuja, naimani ifikapo 2019 kero hii itakuwa historia, “alisisitiza.
Aidha Mhe. Samia amewataka akinamama wajawazito wakiwa tayari kujifungua wakimbilie hospital ama vituo vya afya badala ya kuendekeza masuala ya kishirikina suala linalosababisha vifo kwa mama na mtoto.
Pia aliwaomba ,watumie vituo vya afya kunusuru vifo vya akinamama na watoto.
Akizungumzia tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji alizitaka Jamii hizi Mbili za wakulima na wafugaji waheshimiane.
Akitolea ufafanuzi juu ya kudhibiti tatizo hilo, naibu waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega alisema, NARCO inaanzisha maeneo ya wafugaji na imetenga heka 100,000 ambapo ng’ombe watahamishia malisho ndani ya Narco.
“Miezi mitatu ng’ombe mmoja atalipiwa sh. 10,000 na ukiisha muda huo unaanza mkataba upya”alielezea.kuwa njia hiyo itapunguza ongezeko la mifugo hiyo.
Ulega alieleza kuwa itakuwa ni ofa kwa wafugaji kunenepesha ng’ombe wao kwenye shamba hilo la serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.