Mkuu wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo, ametimiza agizo la Waziri Mkuu kwa kukabidhiMadawati 305,Viti na meza 221 kwa shule mbalimbali za Halmashauri ya Chalinze .
Hatua hiyo ni Utekelezaji wa Maagizo ya Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa aliyoyatoa Desemba 7,mwaka huu kwa Wakuu wa Mikoa la Kusimamia ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa na Madawati ili Wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato Cha kwanza kuingia Mashuleni ifikapo Februari 28 mwaka 2021.
Akizungumza wakati akiwa Kikaro Sekondari -Miono, mhandisi Ndikilo alieleza ,Halmashauri hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa Viti na Meza 650, vyumba vya Madarasa 13.
"Tatizo la Viti na Meza 650 na Uhaba wa vyumba 13 vya madarasa limekwisha kwenye Halmashauri hii Mmeweka Mikakati Mizuri ya kukamilisha ujenzi wa madarasa hapa, ;Hadi sasa mna upungufu wa Viti na Meza 61 huku Mbunge Ridhiwani Kikwete ametoa fedha Sh. Milioni 3.6 kumaliza Upungufu huu, Ujenzi wa Maboma 17 unaendelea na utakamilika mapema" Hongereni sana Chalinze Alisema Ndikilo.
Pamoja na hayo,Ndikilo alitoa Wito kwa Wakuu wa Wilaya kuendelea kusimamia ujenzi wa Madarasa kwenye Wilaya zao na Amewataka wataalamu kutoka Sekretarieti ya Mkoa kutoka maofisini kwenda kusimamia ujenzi wa Miundombinu hiyo.
Aidha alifafanua, mkoa huo umefaulisha wanafunzi 30,212 sawa na asilimia 86.9, Halmashauri ya Chalinze pekee imefaulisha wanafunzi 4,965 kwa mwaka huu na wote watapaswa Kuingia shuleni Januari 2021.
Akisoma Taarifa Mkuu wa Wilaya hiyo, Zainabu Kawawa alifafanua,
Wilaya hiyo imejipanga kumalizia ujenzi wa Maboma 17 kupitia Sh. Milioni 100 zilizotolewa na Halmashauri ya Chalinze na wamepanga kuanza ujenzi wa Vyumba vya madarasa 21 kwa ajili ya mwaka 2022 .
Ridhiwani alibainisha, Maelekezo ya Waziri Mkuu wameyasimamia na kuyatekeleza chini ya Uongozi wa Ndikilo na Zainab Kawawa na kudai Chalinze ya Sasa Hakuna Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari na Msingi atakayekaa chini.
Ridhiwani alielezea, Umaliziaji wa Madarasa 17 yanayohitajika kuwa tayari kabla Shule hazijafunguliwa nao unaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.