Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa,LT.Josephine Mwambashi ,ameagiza wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuwashirikisha wananchi hatua ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuondoa kigugumizi cha maswali kwa wananchi hao.
Aidha amewaasa wananchi na viongozi mbalimbali, kuwaunga mkono wawekezaji hususan wazawa ili kuinua sekta ya uwekezaji nchini.
Akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji Mlandizi-Mboga ,unaotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dar es salaam na kugharamiwa na Serikali Kuu, kwa sh.bilioni 17 .79,Mwambashi alisema kila mwananchi ana haki ya kujua maendeleo ya miradi hiyo.
"Niwaagize DAWASA toeni taarifa kwa watendaji wa ngazi za vijiji,kata mmoja ana nafasi yake ,katika Kijiji,kata ,wilaya ,ili kupitia vikao vyao watoe taarifa kwa wananchi wao"alifafanua Mwambashi.
Nae afisa Mtendaji Mkuu DAWASA , Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa taarifa ya mradi huo wa maji anabainisha ujenzi ulianza 2019 lengo upatikanaji wa maji.
Luhemeja alifafanua kwamba ,hadi sasa umefikia asilimia 95 na zimeshatumika bilioni 13 utanufaisha wananchi zaidi ya laki moja.
Awali akipokea mwenge wa Uhuru eneo la Bwawani kutokea Mkoani Morogoro Mkuu wa mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge alisema mwenge huo ukiwa mkoani humo utakagua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 87 yenye thamani ya bilioni 57.311.5.
Alieleza, utatembelea miradi minne,miradi tisa itawekwa mawe ya msingi,14 itazinduliwa na 60 kukaguliwa kwenye wilaya Saba na halmashauri tisa .
Ukiwa wilayani Bagamoyo, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Abdallah alibainisha mwenge utatembelea miradi 14 ikiwa 7 ni ya kikampeni na mingine 7 ya kimaendeleo,yenye thamani ya bilioni 22.
Mwenge huo pia ulifungua mradi wa Msolwa Hotel uliogharimu bilioni 1.235.2 hadi kukamilika ,na kutoa ajira 19 hadi sasa, mradi wa barabara mzunguko Bwilingu wenye thamani ya bilioni 1.1 na kituo cha afya Lugoba ambapo umekagua na kuangalia shughuli za mapambano dhidi ya Ukimwi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.