• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

DC Komba awahimiza Wananchi na Watumishi wa Mkoa wa Pwani Kutekeleza kwa Vitendo maono ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Posted on: May 26th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba, amewahimiza wananchi pamoja na watumishi wa Mkoa wa Pwani kutekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika sekta ya kilimo.

Amesema wananchi wanapaswa kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika mkoa huo kwa lengo la kujikita kwenye kilimo chenye tija na kuimarisha ushindani chanya miongoni mwao, ili kuongeza uzalishaji na hatimaye kuufanya Mkoa wa Pwani kuwa kinara wa kilimo cha mazao ya ufuta, mbaazi, korosho na choroko hapa nchini.

Luteni Kanali Komba alitoa kauli hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, katika mkutano wa wadau wa tasnia ya ufuta na mbaazi uliofanyika katika ukumbi wa FDC uliopo Ikwiriri, wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Mkutano huo uliandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU).

“Tuzitumie fursa zote zilizopo kama vile ardhi, mbolea na nguvu kazi ya watu wetu ili kuongeza uzalishaji. Tushindane kwa uzalishaji bora kati yetu ili Mkoa wa Pwani uwe mfano wa kuigwa na mikoa mingine nchini,” alisema Mheshimiwa Luteni Kanali Komba.

Aidha, alisema kuwa Serikali imefanya juhudi kubwa kuwawezesha wakulima, hasa katika upatikanaji wa mbolea na masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuongeza kipato cha wakulima na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Katika hatua nyingine, aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Pwani kujikita katika kilimo cha mazao yote ya biashara yanayolimwa katika mkoa huo, na kuepuka ubaguzi wa mazao, kwa kuwa ardhi ya mkoa huo inaruhusu kilimo cha aina mbalimbali.

Vilevile, aliwahimiza wakulima kujiepusha na uuzaji holela wa mazao yao, na kusisitiza matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani pamoja na mizani ya kidigitali kupitia Vyama vya Msingi (AMCOS), kuanzia hatua za awali. Alisisitiza pia umuhimu wa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake katika kulinda maslahi ya wakulima.

Kwa upande wake, Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Pwani, Bw. Mutaabazi, alipokuwa akitoa mwongozo wa mauzo ya ufuta na mbaazi kwa msimu wa mwaka 2025/2026, alisema kuwa Vyama vya Msingi vya Ushirika pamoja na watunza maghala wanapaswa kuzingatia viwango na ubora wa mazao kwa kuweka madaraja kuanzia ngazi ya mkulima. Pia alisisitiza matumizi ya mizani ya kisasa pamoja na utoaji wa risiti kwa kila muamala, ili kuweka kumbukumbu sahihi kwa wakulima.

Naye Meneja Mkuu wa CORECU, Bw. Hamis Mantawela, akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya ukusanyaji na uuzaji wa ufuta na mbaazi kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu wa mwaka 2025/2026, alisema kuwa maandalizi ya vitabu vya mazao (shajala) yamekamilika na vinapatikana katika ofisi za CORECU makao makuu Kibaha, tawi la Kibiti, na katika ofisi ya Chama cha Msingi Kigoma AMCOS wilayani Mkuranga.

Aliongeza kuwa, kwa upande wa vifungashio, CORECU imeratibu upatikanaji wa magunia 400,000 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za ufuta na mbaazi, pamoja na kusambaza mizani 135 ya kidigitali kwa AMCOS zote zinazokusanya mazao, ambapo kila chama kimepatiwa angalau mzani mmoja.

Akitoa taarifa ya uzalishaji, Afisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani, Bw. Jerry Abel, alisema kuwa kwa mwaka wa kilimo 2024/2025, mkoa uliweka lengo la kuzalisha tani 22,000 za ufuta na tani 500 za mbaazi, lakini uzalishaji halisi ulikuwa tani 13,053 za ufuta na tani 298 za mbaazi.

Kuhusu mipango ya kuongeza uzalishaji kwa msimu ujao, Bw. Abel alisema kuwa CORECU itaendelea kusambaza mbegu bora za ufuta na mbaazi, wakati Halmashauri zitaendelea kutoa elimu kupitia mashamba darasa, kusimamia usambazaji wa mbegu bora, na kuhakikisha upatikanaji wa masoko pamoja na kuanzisha mashamba ya mbegu ili kuongeza tija.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC Komba awahimiza Wananchi na Watumishi wa Mkoa wa Pwani Kutekeleza kwa Vitendo maono ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

    May 26, 2025
  • Tangazeni Miradi ya Serikali : Msigwa

    May 24, 2025
  • Katibu Tawala Mkoa wa Pwni afunga rasmi Mashindano ya UMITASHUNTA Nganzi ya Mkoa

    May 24, 2025
  • Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Apokea Majiko ya Gas 200 kwa ajili ya Watumishi Wapya

    May 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.