Awamu ya kwanza ya ujenzi wa miundombinu ya Kongani ya kisasa ya viwanda "Modern Industrial Park" iliyopo Disunyara, Mlandizi Kibaha mkoani Pwani (KAMAKA) imefikia asilimia 93 ya utekelezaji.
Mradi huo unaotarajia kugharimu shilingi trilioni 3.5 hadi kukamilika, unatarajia kukamilisha awamu hiyo ya kwanza Februari 2024.
Hayo yamebainika katika ziara ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji aliyetembelea kongani hiyo ili kujionea maendeleo ya hatua za utekelezaji na changamoto zilizopo ili kuzibeba na kwenda kuzifanyia kazi kupitia mawaziri wa kisekta.
Taarifa za utekelezaji zimeeleza kuwa katika kiasi hicho cha shilingi trilioni 3.5, bilioni 122.4 zitajenga miundombinu ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo hadi sasa sh. bilioni 35 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo na gharama zinazohusiana na uwekezaji huo.
Aidha Kijaji amesema ujenzi wa viwanda na kongani za kutosha nchini utawezesha kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana wa kitanzania.
Akizungumzia changamoto za kongani hiyo, Kijaji amesema zipo ambazo zimeanza kufanyiwa kazi na akaahidi kukaa na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa ili kuangalia namna ya kufanikisha ombi la ujenzi wa barabara iendayo kwenye Kongani hiyo.
Aidha, Waziri Kijaji amempongeza mwekezaji huyo wa ndani KAMAKA Co.Ltd kwa kuthubutu na kuwa na uthubutu wa uwekezaji huo mkubwa.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameeleza kuwa barabara ya kuanzia Makofia -Mlandizi -Mzenga -Vikumburu -Mloka ni muhimu kwani inapitia eneo la uwekezaji na lenye miradi ya kimkakati.
Kunenge ameomba kuwa wakati ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ukianza, uanzie Mlandizi kwa maslahi mapana ya eneo hilo.
Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa kuhusu changamoto ya maji, alishaongea na waziri wa maji Jumaa Aweso ambae aliahidi kufika kwenye kongani hiyo kujionea uhalisia wa tatizo.
Akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa Afriq Engineering and Construction Campany Liited Mhndisi Charles Bilinga alisema makadirio ya awali yamaonesha kuwa ajira zisizopungua 200,00 zitatokan na mradi huo ulioanza oktaba 2021 kwa wakazi wa maeneo ya jirani na Kongani ambapo ajira za moja kawa moja zinakadiriwa kuwa 30,000 na pato la serikali litaongezeka kupitia kodi mabalimbali
Mhandisi bilinga alisema gharama za mradi huo hadi kukamilika ni Trilion 3.5 .
Nae afisa Fedha na Masoko wa Turnkey Real Estate, Tumaini Kabengula, ameeleza kuwa mpaka sasa kuna mikataba 1o ya ununuzi wa Viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda , Kuna viwanja 24 vilivyoshikiriwa vikisubiri kusainiwa kwa mkataba , wawekezaji watatu wamekwishaanza hatua za awali za ujenzi na wengine watano waliosani mikataba wataanza mwaka huu.
Alisema wawekezaji waliotembelea kongani kwa nia ya kuwekeza ni 58 wakitokea nchi za India, China ,Uturuki ,Sudan ya Kusini . Afrika ya Kusini ,Rwanda ,Somali, Pakistan,Yemen, Falme za Kiarabu,Misri, Canada ,Uganda, Kenya na Tanzania.
"Mradi ulianza kutekelezwa oktoba 2021 kwa awamu ya kwanza kwenye ujenzi wa lango kuu na uzio, kituo cha Polisi, jengo la Utawala, Ofisi na jengo la makazi ya wafanyakazi wa Zimamoto, Zahanati, kituo cha Umeme wa megawatt 54 , mfumo wa barabara za nje na ndani na umefikia asilimia 93," alibainisha Mhandisi Bilinga
.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.