Katibu Tawala Mkoa Pwani Dkt Delphine Magere amewaatka watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufanya kazi kwa weledi mkubwa huku wakizingatia kanuni sheria na Taratibu za utumishi wa umma.
Hayo aliyasema mwanzoni mwa wiki hii wakati akijitambusha kwa watumishi hao baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa baada ya Katibu atawala aliyekuwepo Bibi Theresia Mmbando kumaliza Muda wake katika Utumishi wa umma.
Dkt Magere aliwataka watumishi hao kuoa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yao kwa lengo la kuuletea Mkoa maendeleo
“Watumishi wote kwa pamoja tukiwa na Umoja na tukiwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yetu tutaweza kufanikiwa kwa mafanikio makubwa hivyo rai yangu kwenu ni tupendane ,tuthaminiane na tushirikiane watumishi wote” alisema Dkt Magere
Nae kwa upande wake katibu tawala aliyemaliza muda wake wa Utumishi wa Umma Bibi Theresia Mmbando amewashukuru watumishi hao kwa kumpa ushiririkiano Mkubwa kwa kipindi chote alichofanya nao kazi,
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watumishi wote wa ofsi hii pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa huu, kwa ushirikiano wenu niliweza kufanyakazi yangu wa weledi na Amani na shukrani za pekee nimpatie Mh. Mkuu wa Mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo kwa ushirikiano wake na alikuwa mshauri wangu mkubwa” alisema mama Mmbando.
Mama Mmbando amewataka watendaji wote wa mkoa pamoja na Halmashauri kutoa ushirokiano kwa katibu Tawala Dkt Magere ambae amekanza rasmi kazi mwanzoni mwa wiki hii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.