Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahil Geraruma, ameiasa jamii kulinda na kuhifadhi tanki la Kisima na kujiepusha na jambo lolote linaloweza kuleta madhara kwa watumiaji.
Akizindua mradi wa tanki la maji katika Zahanati ya 830 KJ Kibiti Mkoani Pwani ambao umekamilka kwa asilimia 100 na ulio tayari kutoa huduma ndani ya jamii inayoizunguka, Geraruma amepongeza usimamizi mzuri katika kutekeleza mradi huo.
Awali akisoma taarifa ya mradi, Kapt. Yusuph Matias Masalu wa 830 KJ Kibiti alisema kikosi kilianza jengo la muda la Zahanati Lakini baadae makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kutumia fedha za maendeleo ya mwaka wa fedha 2020-2021.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia ufadhili wa Shirika la “global A Network” linalotoa msaada wa kuchimba visima virefu Kibiti kwa kushirikiana na Wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) wameweza kutekeleza mradi huo pamoja na visima vingine 19 vyenye thamani ya sh. milioni 380 wilayani hapa”. Alisema Kapt. Masalu.
Kuhusu thamani ya ujenzi wa mradi huo, Masalu alibainisha kuwa wafadhili hao na RUWASA walifanya utafiti wa maji chini ya ardhi na kuchimba kisima hicho ,chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 11,300 kwa saa na urefu wa mita 93 kilichogharimu milioni 20 .
Alieleza, kikosi hicho kimetumia milioni 15.1 Kwa Ajili ya kupima wingi, ubora wa maji, kujenga mnara, kununua tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 10,000, kununua na kufunga pampu kwa Lengo la kutoa huduma ya maji.
Mkuu wa wilaya ya Kibiti, kanal Ahmed Abbas alisema mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani humo utapitia miradi 15 yenye thamani ya sh.milioni 809.3 na kukimbizwa km.110 kwenye kata tano.
Miradi mingine iliyopitiwa ni Pamoja na ujenzi wa vivuko vitatu kwenye bonde la Nyarwanza, ujenzi wa madarasa matatu kwa fedha za Uviko 19, mradi wa madarasa matatu katika Shule ya Sekondari Mtawanya kwa fedha za mapato ya ndanimradi wa kituo cha afya Mjawa na shamba la kilimo Cha korosho na ufuta lenye ukubwa wa hekari 70.
Mwenge wa Uhuru Mei 3 mwaka huu ,unatarajiwa kupokelewa wilaya ya Mkuranga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.