Mkuu wa wa mkoa wa Pwani , Mhandisi Evarist Ndikilo ameweka jiwe la Msingi katika katka kituo cha afya Ikwiriri Rufiji ambacho kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles kabeho alikataa kuweka jiwe hilo Julai 2018, kutokana na mkanganyiko wa taarifa baina ya Wilaya na Mkoa.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la msingi, Ndikilo alisema walichukua hatua ya kufanya uchunguzi kupitia vyombo vya dola na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) na kubaini hakuna wizi uliofanyika kwenye ujenzi huo.
“Kama kuna miundombinu kwa baadhi ya majengo haijakamilika iangaliwe namna ya kuikamilisha , katika vituo vyote vilivyojengwa mkoni hapa”. Alisema Ndikilo.
Pia alieleza kuwa Mkoa ulipokea bilioni 8.2 kwa ujenzi wa vituo vya 18 na ukarabati wa hospitali ya wilaya na bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali tatu za wilaya.
Aidha Mhandisi Ndikilo aliwataka watumishi wa afya kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi wanaofuta huduma hiyo na kuacha lugha chafu.
Naye Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohammed Mchengelwa aliishukuru Serikali ,kwa kuimarisha sekta hiyo na kwa kutoa zaid ya sh. Million 320 kuboresha sekta hiyo Wilayani Rufiji.
Awali , Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Mjwayo alibainisha , kuwa kama Wilaya wamejiridhisha , kuwa kama Wilaya wamejiridhisha hivyo alimuomba Mkuu wa mkoa kufanya zoezi hilo. Pia alimpongeza kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2018 Charles Kabeho kwa ufuatiliaji wake makini wa thamani na ubora wa miradi wakati wa mbio za Mwenge hali iliyosababisha kila Halmashauri kuwa makini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.