Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Pili Mnyema ameipongeza Halmashauri ya Mji Rufiji kwa ukusanyaji wa mapato ya zaidi ya asilimia 100 na kusisitiza kwa mwaka huu wa fedha kuendelea kukusanya zaidi ili kuwezesha utejelezaji wa miradi ya maendelea yenye tija kwa wananchi.
Mnyema ametoa pongezi hizo Leo Agosti 26, 2025 Wilayani Rufiji alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani zikilenga ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na watumishi.
"Niwaombe kwa mwaka huu wa fedha tuendelee kukusanya zaidi ili kuendelea kuwahudumia wananchi, kwani makusanyo yatawezesha ukusanyaji wa fedha zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo itayoleta tija zaidi kwa wananchi tunaowahudumia kwani ndio kipaumbele chetu" Alisema Mnyema.
Aidha aliwapongeza kwa ubunifu wa miradi uliwezesha kupata vyanzo vipya vya mapato na kusisitiza kuendelea kuvitunza vyanzo vya zamani.
"Jukumu la ukusanyaji wa mapato ni letu sote, tulifanye kwa weledi ili liweze kuobgeza tija pamoja na utumiaji mzuri wa fedha, usimamizi mzuri wa miradi ya maeneleo kwa uaminifu mkubwa," aliongeza Mnyema.
Pia aliwasisitiza watumishi kufuata misingi ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa unyenyekevu, uadilifu, upendo na kufuata sheria ili kutimiza malengo ya serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.