Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka viongozi wa Halmashauri za Wilaya ya mji wa Kibaha, Mkuranga na Chalize kuadaa mikakati ya kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi va ugonjwa wa Ukimwi.
Ndikilo alisema Halmashauri hizo zimeeleza kuongoza kwa maambukizi mapya ya VVU huku chanzo kikielezwa kuwa ni muingiliano wa shughuli za kiuchumi,
Alisema takwimu za maambukizi kwa Mkoa huo za mwaka 2012 ni asilimia 5.9 na kwamba kimeahuka hadi kufikia asilimia 5.5 kwa mwaka 2017.
Alisema pamoja na kushuka kwa maambukizi lakini bado Halmashauri hizo zinaonekana kuwa na maambukizi mengi sababu sikielezwa kuwa biashara, Viwanda vingi na vituo vya magari makubwa.
Hata hivyo maambukizi kwa wanawake kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu yanaelezwa kufikia asilimia 4.3 huku wanaume wakiwa ni asilimia 3.6.
" Pamoja na takwimu hizi suala la upimaji wa hiari idadi kubwa ya wanaopomwa wanaelezwa kuwa ni wanawake ukilinganisha na wanaume, wanaume wanaonekana kuwa waoga" alisema Ndikilo.
Ndikilo alisema moja ya vikwazo vinavyoelezwa kuchochea maambukizi mapya ni pamoja na mila potofu, ndoa za utotoni na ngoma za usiku.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Delphine Magere aliwataka wanawake kuwa wakwanza kupinga maambukizi mapya kutokana na umuhimu wao kwenye majukumu ya kifamilia.
Akisoma risala ya Watu wanaoishi na VVU mmoja wa wawakilishi watu hao Elizabeth Hassan alisema kikwazo kilichopo katika kundi hilo ni baadhi ya Watu wanaoishi na VVU kusitisha kutumia dawa za kurefusha maisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.