• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Halmashuari kuu ya CCM Mkoa Pwani ,imeridhishwa na usimamizi wa utekelezaji wa maendeleo

Posted on: November 22nd, 2023

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani, imeridhishwa na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaofanywa na Serikali mkoa ambao umetekelezwa kwa asilimia 98 :";pamoja na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka trilioni 1.19 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Aidha imetoa rai kwa Serikali mkoa , kuhakikisha inaendelea kutekeleza kwa kasi miradi ya maendeleo ambayo bado haijakamilika ili ifikapo Disemba 2024 iwe imekamilika.

Hayo yalijiri wakati Kamisaa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) March 2021-Juni 2023, katika kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoani humo.

Kunenge alijinasibu kuwa wanatekeleza ilani kwa vitendo ,na kuahidi kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo ambayo ipo mbioni kukamilika .

Akielezea utekelezaji upande wa miundombinu alieleza ,ujenzi wa barabara kutoka Kibaha- Chalinze- Morogoro km 220 kuwa njia nne (Express way) mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa EPC +F Engineering, Procurement, Construction and Financing ,ujenzi unatekelezwa na Mwekezaji.

"Usanifu wa awali wa mradi huu kuanzia Kibaha hadi Morogoro umeshafanyika , kwasasa Mwekezaji anatafutwa ili ujenzi uanze"

"Barabara hii itapunguza changamoto ya msongamano wa magari na kupunguza ajali ambazo huwa ukijitokeza "alieleza Kunenge.

Hata hivyo Kamisaa huyo alieleza, miradi mingine inaendelea kwa kiwango cha lami katika barabara kuu na barabara za mkoa ikiwemo Kibaha - Mapinga km 23.

SEKTA YA VIWANDA

Idadi ya viwanda imeongezeka kutoka viwanda 1,472 mwaka 2022/2023 viwanda 120 ni vikubwa , 120 vya kati, 271 vidogo na 1,014 vidogo sana.

Kunenge alieleza, kunaongezeko la viwanda 53 ambavyo viwanda 30 ni vikubwa ,ujenzi wa viwanda vipya 15 vinaendelea.

UTALII

Utalii mkoa una vivutio 87 vinavyojumuisha mambokale, misitu ya Hifadhi ya mazingira asilia ,mapori ya akiba ya selous na Wamimbiki ,hifadhi za Taifa za Nyerere na Saadan na fukwe nzuri za bahari.

Ongezeko la watalii limepelekea mapato kuongezeka kutoka sh Bil 9,439,529,840 hadi sh.Bil 14,888,903,208.

Kunenge alieleza ,Mafia imejifungua na kujitangaza kwa utaliii wa Uchumi wa Bluu na Samaki papapotwe samaki anaevutia na kuwa kivutio kikubwa , na aliongeza wanaendelea kuutangaza mkoa kwa utalii uliopo.

NISHATI

Ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere JNHPP 2115 MV, utekelezaji umefikia asilimia 93 na unatarajia kukamilika Juni 2024.

Alieleza, njia ya kusafirisha Umeme ya 400 KV kutoka JNHPP hadi Chalinze 160 KV na usf 51 m,sh 39 Bilioni sawa na Jumla ya Bilioni 158 utekelezaji asilimia 99 ,utakamilika disemba 2023.

Kituo cha kupoozea umeme Chalinze Bilioni 128 utekelezaji umefikia asilimia 85.5 utakamilika disemba 2023.

MAJI

Mkoa una vijiji 417 ,mitaa 73 hadi sasa vijiji 331 vimepata maji yenye kujitosheleza, vijiji 57 vina huduma ya wastani sawa na asilimia 79.3 ya wakazi wote wa Mkoa ikiwa asilimia 77 ya wakazi wa Mkoa ikiwa asilimia 77 ya wakazi waishio Vijijini na asilimia 85 ya wananchi Vijijini.

AFYA

Kunenge alieleza, kuna ongezeko la upatikanaji wa dawa, vifaa tiba ,vitendanishi kutoka asilimia 92 kwa kipindi cha februari- machi 2021 hadi asilimia 93.2 kipindi cha april- mei 2023.

Tunaangalia bajeti inayoletwa kutatua changamoto,tunatekeleza , kuna miradi iliyokamilika ,na ipo ambayo haijakamilika,tunajinasibu tunatekeleza kwa vitendo na anayetaka kuyaona na kujifunza aje mkoa wa Pwani ajionee" alieleza Kunenge.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani, Mwinshehe Mlao alieleza , miradi imetekelezwa na amepongeza usimamizi mzuri unaofanywa kwenye miradi ya maendeleo.

Alitaka mkoa kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi ambayo inaendelea kutekelezwa .

Mlao alisema Chama na Serikali ni kitu kimoja ,hivyo alihimiza ushirikiano baina ya Chama na Serikali ili kuinua maendeleo na uchumi kwa wananchi.

Kwa upande wake ,Katibu wa CCM Mkoani Pwani, Bernard Gatty alieleza, kamati ya siasa ya mkoa ilifanya ziara katika wilaya zote kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama na kusema utekelezaji umefikia asilimia 98.

Alieleza kwa utekelezaji huo ,wanaimani na ushindi kwa uchaguzi ujao wa Serikali ya mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

"Rais Samia Suluhu Hassan ametutendea haki kutuletea fedha nyingi, watalaam wamefanya kazi yao na Serikali kusimamia kikamilifu, hatuna shaka kujibu hoja kwa wapiga kura wetu,"alisisitiza Gatty.


Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.