Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewataka Watendaji wa Halmashauri zote za mkoa huo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ili kuisaidia serikali kutekeleza majukumu yake.
Kunenge ametoa agizo hilo leo Juni 20, 2023 kwenye vikao vya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG vilivyofanyika kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Mkuranga na Kisarawe mkoani humo.
Amesema suala hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Mikoa yote nchini kumpatia taarifa ya ukusanyaji wa mapato kila wiki hivyo akaelekeza kuwa ili kufanikisha agizo hilo, kasi ya ukusanyaji wa mapato lazima iongezeke.
“Mwaka jana Mkoa wetu ulikuwa wa tatu kwa ukusanyaji wa mapato ambapo tulifikia asilimia 108, sasa mwaka huu nataka tuwe wa kwanza tuondoke kwenye nafasi hii na ili tufanikiwe lazima tushirikiane tubuni na kuanzisha vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vitaupaisha mkoa wetu kwa sababu mahitaji ya wananchi yanaongezeka na huduma za serikali pia zinahitajika hivyo ni muhimu kuwa na vyanzo vya mapato vya kutosha,” amesema Kunenge alipokuwa Mkuranga.
Amebainisha kuwa kwa sasa Halmashauri za mkoa huo huku akitaja baadhi na asilimia za ukusanyaji wa mapato walizofikia hadi sasa kwenye mabano kuwa ni Rufiji (104), Kibiti (79), Mkuranga (91) na Kisarawe (76) na akazitaka kuongeza kasi.
Katika hatua nyingine akiwa Kisarawe Kunenge amewataka viongozi wa Halmashauri kutenga na kuanisha maeneo yote ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Pia amewaelekeza kufanya mapitio ya vyanzo vya mapato ili kuziboresha zenye tija na kuanzisha vipya bila kuleta usumbufu wa aina yoyote yenye bughdha kwa wananchi.
“Fanyeni uchambuzi na kubaini vyanzo vilivyo imara mviongezee nguvu ya kuviimarisha ili viweze kuongeza mapato lakini visiwe sumbufu kwa kusababisha kero kwa wananchi,” alielekeza na kutahadharish
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.