Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.Selemani Jafo amefanya ziara ya siku moja kutembelea viwanda katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ikiwa ni pamoja na kusikiliza Changamoto za wawekezaji.
Dk. Jafo amesema tayari alishatoa maelekezo kila Mkoa kutenga maeneo ya uwekezaji jambo ambalo kwa mkoa wa Pwani tayari wameshaanza kufanyia kazi.
Amewahakikishia wawekezaji wanaotaka kuwekeza hapa nchini kwamba wako salama na Mazingira yameimarishwa katika Taasisi zote zinazohusika.
Katika ziara yake hiyo Dk. Jafo amekagua shughuli zinazofanyika katika kiwanda Cha kuzalisha dawa za kuua mazalia ya mbu (viuwadudu) kilichopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Akiwa kiwandani hapo Waziri huyo amesema Halmashauri zote hapa nchini zinatakiwa kuona jambo la muhimu kupata dawa hizo na kuuza mazalia ya mbu kwenye maeneo yao badala ya kuruhusu wananchi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa huo.
Pia ameelekeza uongozi wa NDC kufanya kampeni maalumu ya kutangaza dawa hiyo kwa wananchi Ili waweze kuitumia kwenye maeneo yao na.kupinguza jasi ya uwepo wa wagonjwa wa malaria.
Akiwa katika eneo la Uwekezaji la Modern Industrial park maarufu Kamaka Dk. Jafo ameahidi kuhakikisha vikwazo kwa wawekezaji vinatatuliwa kwa haraka Ili wanaohitaji kuwekeza wapate fursa hiyo.
Waziri Dk.Jafo pia meahidi kufuatilia upatikani wa kituo cha treni ya mwendokasi (SGR) katika eneo la Kwala ili kurahisisha shughuli za usafirishaji.
Kadhalika Dk.Jafo amesema atamuomba Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko kusaidia, upatikanaji wa umeme wa uhakika unaohitajika wa Megawatts 54 katika eneo la Modern Industrial Park.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akizungumza katika ziara hiyo amesema kupitia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewezeaha kuwepo kwa mazingira ya rafiki kwenye huduma huduma zote za uwekezaji katika eneo moja.
Akiwa katika eneo hilo la Kamaka ambalo lina ukubwa wa la hekari 1077 ambalo litatumika katika shughuli za uwekezaji ameahidi kuendelea kumkumbusha Waziri huyo kuhusiana na upatikanaji wa umeme wa kutosha katika eneo hilo kuondoa vikwazo kwa wakezwji pindi uzalishaji utakapoanza.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mhe Michael Mwakamo amesema amefurahishwa na ujio wa waziri wa Viwanda na Biashara kwani aweza kuona haja kuwa na kutuo cha SGR eneo la Viwanda la Sinotan--Kwala.
Mkurugenzi wa Sinotan Jason Huang amesema Kwa Sasa changamoto iliyopo katika eneo hilo ni upatikani wa umeme na Maji ya uhakika, ambapo Mhe waziri ameahidi kulifanyia kazi kwa haraka akishirikiana na Mamlaka husika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.