Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo amekabidhi sh. Milion 50 kwa walimu wa shule ya Sekondari ya Tumbi iliyopo Kibaha ikiwa ni kutimiza ahadi iliyotolewa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Dk. Mpango alitoa ahadi hiyo hivi karibuni alipofika katika shule hiyo kupanda miti ambapo alifurahishwa na matokeo ya kidato cha nne baada ya wanafunzi 40 kupata ufaulu wa daraja la kwanza.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo Dk Jafo amesema fedha hizo zilizotolewa na Dk Mpango zinatakiwa kuongeza motisha zaidi kwa walimu katika ufundishaji na kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kufaulu.
Amesema Tumbi ni shule ya kwanza hapa nchini walimu kupatiwa zawadi kutokana na wanafunzi kufanya vizuri badala yake fedha zimekuwa zikitolewa na serikali kwa ajili ya maboresho ya shule miundombinu na vifaa na si kwa walimu kama ilivyotokea.
"Fedha hizi hamkupata kwa upendeleo mnastahili kupata kutokana na kazi mlioifanya kupata wanafunzi 40 waliofaulu kwa daraja la kwanza kwa idadi hii ni kubwa sana ongezeni juhudi zaidi mulitangaze Shirika la Elimu na Mkoa" amesema Jafo.
Nae Katibu Tawala wa mkoa huo Rashid Mchatta kwa upande wake amewapongeza walimu hao kwa kazi wanayoifanya na kuinua ufaulu kwa mkoa huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Anathe Nnko ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukarabati majengo kwenye shule zilizo chini ya Shirika hilo.
Mkuu wa shule hiyo Fidelis Haule amemshukuru Makamu wa Rais Dk Mpango kwa kutekeleza ahadi kwa walimu ambayo aliahidi.
Akitoa taarifa ya Shule Haule amesema shule hiyo ni shule ya kawaida ola imekuwa ikifanya vizuri kwa kuongezaka kwa ufaulu wa daraja la kwanza ambapo kwa miaka minne mfilulizo ambapo kwa mwaka 2019 daraja la kwanza walikuwa wanfunzi 8, mwaka. 2020 daraja la kwanza wanafunzi 23, mwaka 2021 daraja la kwanza wanafunzi 28 na mwaka 2022 daraja la kwanza wanafunzi 40.
Haule amesema shule hiyo imeendelea kuwa ya pili kimkoa kwa shule za Serikali ikitanguliwa na Shule ya Sekondari ya wavulana Kibaha kwa miaka mitano mfululizo kuanzia 2018
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.