Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge leo amepokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 katika Mkoa wa Pwani ukitokea katika Mkoa wa Morogoro.
Kunenge amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigella pamoja na vijana wakimbiza Mwenge sita kitaifa wakiongozwa na Luten Josephine Poul Mwambashi.
Akipokea Mwenge wa Uhuru Kunenge amebainisha kuwa jumla ya miradi 87, yenye thamani ya shilingi Bilioni 57,311,572,720 itatembelewa katika Halmashauri zote tisa katika Wilaya saba za Mkoa wa Pwani.
Katika miradi hiyo miradi tisa itawekwa mawe ya Msingi, miradi 14 itazinduliwa, miradi minne itafunguliwa na miradi sitini itakaguliwa.
"Miradi yote hiyo itatekelezwa Kwa ushirikiano Mkubwa wa Wananchi, Halmashauri, Serikali kuu pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, pia miradi hiyo imezingatia kaulimbiu isemayo "Tehama ni Msingi wa Taifa endelevu tuitumie Kwa usahihi na uwajibikaji", amesema Kunenge.
Aidha kauli mbiu hiyo imeambatana pia na jumbe za kudumu za Mwenge wa Uhuru 2021 wa kuitokomeza rushwa, mshikamano wa Taifa, kujenga jamii imara Kwa kuchagua lishe Bora, kupambana na malaria na elimi juu ya dawa za kulevya.
Pia Kunenge amebainisha kuwa katika Mkoa wa Pwani matumizi ya Tehama yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo hadi Sasa Pwani inajumla ya mifumo ya Tehama 29 inayotumika katika shughuli mbalimbali za Serikali.
Ametaja baadhi ya mifumo hiyo kuwa ni pamoja na mifumo ya ukusanyaji wa fedha katika Serikali za mitaa, mfumo wa usimamizi wa taarifa za Hospitali, mfumo wa usimamizi wa elimu Msingi na mfumo wa usimamizi wa taarifa za sekta ya kilimo.
"Mifumo hii imesaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali Kwa utunzaji wa taatifa muhimu", Amesema Kunenge.
Aidha amesema kutokana na kukua Kwa Tehama kumeongeza pia watu wanaotumia vibaya na kusababisha upotevu wa fedha na kufanya udhalilishaji na vitisho sambamba na ongezeko la changamoto ya malezi.
Pamoja na changamoto hizo Kunenge amesema mkoa wa Pwani umejipanga Kwa kushirikiana na Wananchi, wadau wa maendeleo pamoja na Serikali kunitumia Tehama katika Mkoa wa Pwani Kwa maendeleo endelevu.
Kunenge amekabidhi Mwenge Maalum wa Uhuru 2021, Kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah, ambapo miradi mbalimbali itatembelewa na kuzinduliwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.