• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Kabeho asisitiza kuwa huduma za Afya ziboreshwe

Posted on: July 19th, 2018

Bohari ya madawa (MSD), imeelekezwa kufanya jitihada za kupeleka vifaa tiba vitakavyokidhi mahitaji ,katika kituo cha Afya Kerege kilichopo Bagamoyo, Mkoani Pwani ,ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa vifaa tiba .


Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu ,Charles Kabeho a ,Kerege wilayani Bagamoyo wakati alipokuwa akikagua na kujionea shughuli za mapambano dhidi ya Ukimwi katika kituo hicho .


Pia alieleza adhma ya serikali ni kuona vituo   vya afya vinaongezekana huduma za afya zinaboreshwa hivyo MSD ihakikishe inasambaza vifaa hivyo na madawa ili kuendana na malengo ya serikali .


Akizungumzia suala la ugonjwa wa Ukimwi ,aliitaka jamii kujitambua kwa kupima afya zao na ambao walishagundulika kuwa na VVU waendelee na dawa bila kupuuzia masharti ya waatalamu wa afya.


Katika hatua nyingine Kabeho alisisitiza kuwa ,UKIMWI bado upo hivyo kila mmoja anawajibu wa kujali afya yake na kupambana na maambukizi mapya.


Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kerege ,mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Silivia Mamkwe alisema hadi sasa mradi huo umegharimu kiasi cha sh.milioni 561 ambapo mil.500 ni fedha kutoka OR-TAMISEMI .


“Kiasi cha sh.mil.44 ni mchango wa halmashauri ,mil.11.353 ni mchango wa wadau ,mil.4.147 wananchi na mil .1.5 kupitia nguvu kazi “.


Silivia alisema, lengo la mradi ni kuboresha huduma za afya ,dharura na upasuaji wa wajawazito ambapo huduma za upasuaji wa dharura zimesogezwa karibu na wananchi kupunguza vifo vya mama na watoto .


Alisema ,mradi ulianza kutekelezwa oktoba mwaka jana na kwasasa majengo matano ,miundombinu mitano vimekamilika kwa asilimia 100,huku wakitarajia kufikia wananchi 8,921.
“Majengo mawili la kuhifadhi maiti na jengo la kufulia yamekamilika kwa asilimia 80” alifafanua.


Akipokea mwenge wa uhuru kutoka Kibaha Vijiji ,Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alhaj Majid Mwanga alisema ,mwenge huo utapitia miradi 12 iliyogharimu sh.bilioni 10.8.
Alhaj Mwanga alielezea, miradi miwili itakaguliwa na miradi kumi itawekewa mawe ya msingi.
Mwenge wa uhuru unaendelea na shughuli zake Mkoani Pwani ,ikiwa umefikia halmashauri ya saba kati ya tisa na wilaya ya tano kati ya saba za mkoani hapo.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.