Kamisaa wa Sensa 2022, Anne Makinda ametoa ufafanuzi kwamba ,siku ya sensa Agosti 23 mwaka huu haitakuwa siku ya mapumziko badala yake kila mmoja ataendelea na shughuli za kimaendeleo ,pia amesema , tarehe 23 itakuwa siku maalum ya kuhesabiwa lakini itaendelea taratibu za kuhesabu madodoso Hadi tarehe 28 agost mwaka huu.
Akizungumza katika Kongamano la viongozi wa dini pamoja na kuzindua tangazo la umuhimu wa ushiriki wa sensa alisema ,kila mmoja ana wajibu wa kujisensa mwenyewe kwa kutambua wajibu ni wa kila mmoja .
"Mkoa wa Pwani na wilaya ya Kibaha Nimejifunza Jambo kubwa kujisensa mwenyewe,kilichobaki agost 23 mwaka huu tuweze kujisensa wenyewe ili kupata takwimu sahihi kwani tukifanikiwa Tanzania itakuwa mpya".
“Anne alisema, wamejiandaa vizuri mno kwa kutumia teknolojia ya kisasa (kishkwambi ) kurahisisha uhifadhi wa taarifa tofauti na sensa za miaka iliyopita.
Hata hivyo ,aliomba watu waweke vitambulisho vyao karibu ili wanapopita makarani waweze kujua idadi ya wenye vitambulisho huku mamlaka husika iweze Kuwa na takwimu halisi ya walivyo navyo na wasio navyo, vilevile ,alitoa Rai kwa jamiii kuacha kuwaficha walemavu na badala yake wahesabiwe ili kupata taarifa sahihi ya idadi na aina ya ulemavu walionao.
Kuhusu Wamachinga wameingizwa katika sensa, Ni kundi muhimu, ambapo Serikali inataka kujua idadi halisi,wenye vitambulisho kwani mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan ni WAMACHINGA kupatiwa vitambulisho vya ujasiliamali.
"Tushiriki kikamilifu, na Baadhi ya maswali yatakayoulizwa na makarani wa Sensa ni elimu ya wanakaya, shughuli zao za kiuchumi, hali ya uzazi, taarifa za vifo na vifo vitokanavyo na uzazi,ajira, makundi maalum"alisema Anne.
Pamoja na hayo ,aliliasa kundi la vijana wakati wakitumia mitandao kuchat pia watumie wasaa huo kuhamasishana kuhusu suala la umuhimu wa Zoezi la sensa ili kutambua vijana waliopo na taarifa zao kuhusiana na suala la ajira.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alieleza, mkoa umejipanga Kuwa sehemu ya mafanikio Kwenye Zoezi la sensa .
Alielezea kwamba ,zaidi ya viongozi wa dini 1,500 kutoka madhehebu na nyumba za ibada mbalimbali wameshiriki kwenye kongamano hilo la viongozi wa dini.
Kunenge alisema, mkoa na wilaya umejiwekea mikakati kuanzia vitongoji ,kata,wilaya na mkoa kutoa elimu ya umuhimu wa sensa kupitia njia mbalimbali ikiwemo mikutano na wananchi,bodaboda,wakufunzi,makarani,matamasha ,kwenye michezo na makongamano .
"Watendaji 143 nao wameudhuria mafunzo ili kupata uelewa wa kusimamia Zoezi la sensa;"Pamoja na vikao viwili vya kamati ya sensa mkoa vimefanyika "alieleza Kunenge.
Kwa upande wake,Mwenyekiti mwenza wa kamati ya Usalama mkoa ambae pia ni Sheikh mkuu mkoa wa Pwani Hamis Mtupa sensa Ni takwa la kidini.
"Mafanikio pia ya kidunia Ni kwasababu ya kujisensa mwenyewe kwahiyo sensa Ni agizo na takwa la kidini ili kujua kesho yako.
Mtupa alieleza kuwa, viongozi wa dini wamelibeba Zoezi hili watahakikisha linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Nae Askofu Emmanuel Mhina alisema kuwa kamati hiyo ilianza kipindi kirefu kufanya maandalizi ya kongamano hilo na hadi sasa wanaona kuna mwelekeo mzuri.
"Tunaona kuna mafanikio makubwa hadi hapa tulipofikia mwitikio ni mkubwa hivyo tunaamini kuwa siku ya sensa wananchi watajitikeza kuhesabiwa"alisema Mhina.
Mchungaji wa Kanisa Anglikana Kibaha Mkoani Pwani Exavia Mpambichile aliwataka Waumini na wakazi wa Mkoa huo kuzingatia maagizo ya Serikali na kujitokeza wakati wa Sensa Ili kupatikana takwimu sahihi itakayofanikisha Serikali kupanga bajeti stahiki .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.