Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge amsema kuwa kanda ya mashariki imedhamilia kuwa kanda ya mfano katika maenesho ya nane nane kwani kanda hiyo imekuwa na bahati na kuwa na fursa nyingi katika seketa mbaklimbli
Hayo ameyasama Agosti 4, 2022 wakati akitoa salama za ufunguzi wa maonesho hayo ya nanenane ambayo yalifunguliwa na Mhe Mizengo Kayanza Peter Pinda Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne.
Akitoa salaam za Mkoa Kunenge ameeleza Kanda hiyo ya Mashariki imedhamiria kuwa Kanda ya Mfano katika Uwekezaji mbalimbali kwani kuna Fursa nyingi za Uwekezaji katika Sekta ya Mifugo, Uvuvi, Madini, Viwanda, Utalii, Kilimo n.k.
Ameeleza kuwa kanda hiyo imedhamiria kuzalisha kwa Tija na inatazama mnyororo wa Thamani wa Uwekezaji wote na kufanya Matumizi bora ya Ardhi ili kupata Tija.
Amemshukuru Mhe Pinda kwa kubali kuwa Mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi huo
"Tumekupendeza uwe Mgeni Rasmi kwa kuwa wewe ni Mkulima Mzoefu na tunajua wakati ukitembelea mabanda hutaangalia tu bali utatoa maelekezo na mapendekezo katika kuboresha Maonesho yetu haya" Ameeleza Kunenge.
Akizungumza kwenye Maonesho hayo Mhe Pinda amesema Kanda hiyo ya Mashariki ni kanda inayokuwa kwa kasi ni kanda ya Kiuchumi. Ameeleza kanda hiyo ina Miundombinu Muhimu ikiwemo Reli ya Mwendokasi, Barbara za Kisasa, Viwanda Vingi na Vyuo vya Elimu vyingi.
Ametaja Mikoa hiyo ya Kanda ya Mashariki ina Idadi kubwa ya wakazi zaid Milioni 13 na kusema ni Soko kubwa ambalo likitumika Vizuri litatusogeza mbele kama Nchi.
Pinda Ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kukuza kilimo kwa kuongeza Bajeti za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo Ameeleza mwaka 2021 kilimo kilichangia Asilimia 61 ya Ajira. "Ni muhimu kusisitiza haya ili tunapokuja kwenye Maonesho ya Nane nane tupate Maarifa, Teknolojia na ujuzi ili tunaporudi kwenye Maeneo yetu tukayatumie" Ameeleza Pinda.
Maonesho hayo ya nanenene na maonesho ya 29 ambayo yanahusisha mikoa ya Dar es salaam,.Pwani, Tanga na Morogoro ambapo wilaya zote 27 na Halmashauri 34 zimeshiriki pamoja na taasisis mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.