Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Nuhu Mruma ameshiriki iftari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na kuwashirikisha watu mbalimbali wakiwemo watoto yatima kutoka vituo vya kulelea watoto.
Katibu huyo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kuandaa furari hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mruma ambaye alimuwakilisha Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber amesema kilichofanyika katika Mkoa huo ni muendelezo wa kile alichofanya Mhe Rais Mach 4 Ikulu.
Amewataka watanzania kuendelea kushikamana na kuwa wamoja na kujali yatima hususani wenye mahitaji katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani huku wakiendelea kufanya ibada kwa utulivu na amani.
Pia Alhaji Mruma amewapongeza Bakwata mkoa wa Pwani kwa kuungana pamoja kutafuta furari na kusaidia makundi yanayostahiki.
Kadhalika Katibu huyo amesema Bakwata wanaendelea kuhimiza utunzaji wa Mazingira sambamba na kukemea mmomonyoko wa maadili Ili kujenga Jamii yenye uadilifu inayoepuka rushwa na maasi.
Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamis Mtupa amesema kinachofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani ni jambo la kuigwa kwakua limegusa wahitaji katika furari hiyo.
Amewataka watu wengine wanaolenga kufuturisha kuiga utaratibu wa Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani amesema furari hiyo ambayo imeandaliwa na Rais imewakutanisha watu mbalimbali wakiwemo watoto yatima.
Hafla hiyo iliambatana na Dua maalumu kwa ajili ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.