Kaya za wanufaika 18,403 wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Mkoani Pwani, wamehitimu na kujiondoa katika mpango huo kufikia Juni 2024.
Akitoa taarifa kikao cha mwaka cha utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), Mratibu wa TASAF Mkoani Pwani, Roselyn Kimaro amesema, taratibu zikikamilika walengwa hao watakuwa wamejiondoa kwenye mpango baada ya kuandaliwa vizuri na sasa wamefanikiwa.
Ameeleza, kaya za wanufaika 18,403 zimehitimu ambapo kaya 17,761 zinazoendelea kunufaika zikiwa ni kaya katika vijiji vipya vya 30.
Hata hivyo ameeleza, mkoa unaendelea na utekelezaji wa shughuli za mpango kwa kipindi cha pili kilichoanza mwaka 2020 kwa lengo la kuendelea kupunguza kiwango cha umaskini kwa kuhakikisha wananchi wanapata mahitaji muhimu.
Roselyn anaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kiasi cha sh.bilioni 40.3.
Mnufaika Ramadhani Selemani amesema,yupo tayari kujiondoa na anaishukuru serikali kupitia mpango huo na kusema unainua maisha ya kaya maskini.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,alhaj Abubakar Kunenge ameipongeza TASAF mkoa kwa usimamizi mzuri wa fedha za utekelezaji mpango na wanafanya kazi kubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.