Kiongoziwa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, ameipongeza Serikalikwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi nasalama, kufuatia uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kijiji cha Kwala,Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Mradihuo, unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA),umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.4 na unatarajiwa kuwa mkombozi kwawakazi 6,407 wa vijiji vya Kwala na Mwembengozi, waliokumbwa na changamoto yamuda mrefu ya ukosefu wa maji safi.
Akizungumzawakati wa uzinduzi, Ussi aliipongeza RUWASA kwa kazi nzuri na kuagizakuhakikisha maji yanasambazwa kikamilifu kwa wananchi wote waliokusudiwa.Alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika kuutunza mradi huo ili uweendelevu kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
“Niwaombe wananchimkaulinde na kuutunza mradi huu; ni fedha nyingi ambazo Serikali inazielekezakuboresha na kujenga miundombinu hii kwa ajili yenu,” alisema Ussi.
Kwaupande wake, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibaha, Deborah Kanyika, alieleza kuwamradi huo umefadhiliwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) na mpango wa P4R,na hadi sasa mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 1.374.7.
Alifafanuakuwa kati ya wananchi 6,407 wanaotarajiwa kunufaika, tayari 1,752wameunganishiwa huduma ya maji majumbani, huku wengine wakihudumiwa kupitiavituo vya kuchotea maji vilivyojengwa kwa ajili ya umma.
Kanyikaalibainisha kuwa chanzo cha maji ni kisima kilichopo katika Kijiji cha MinaziMikinda, chenye uwezo wa kuzalisha lita 43,000 kwa saa. Mradi huo ulianzishwakufuatia uchakavu wa miundombinu ya awali iliyojengwa mwaka 1974, ambayohaikidhi mahitaji ya sasa.
Aliongezakuwa mkataba wa ujenzi ulisainiwa mwaka 2022, na kazi zilihitimishwa Aprili2024, huku mradi ukiwa kwenye kipindi cha matazamio hadi Aprili 30, 2025.Utekelezaji wake umefanywa na kampuni ya JECCS Construction & SuppliersLtd. JV Works Contractors, ambayo ilijenga tanki la zege lenye ujazo wa lita500,000 juu ya mnara wa mita 12, pamoja na vituo vya kuchotea maji.
Akizungumzakwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, alielezakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenyesekta ya maji, na kwamba mradi huu umeongeza kiwango cha upatikanaji wa majiKibaha Vijijini kwa asilimia 5.2, na kufikia jumla ya asilimia 82.
“Lengo la mkoa ni kufikiaasilimia 95 mijini na asilimia 85 vijijini ifikapo mwisho wa mwaka huu,”alisema Kunenge.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.