Kiongoziwa mbio za Mwenge Kitaifa, Godfrey Mzava amezitaka Taasisi za Umma kutangaza zabuni kupitia mfumo wa kidigital wa manunuzi ya umma ambao unasimamiwa na mamlaka ya udhibiti ya manunuzi ya umma (PPRA),ili kuondoa tabia za kukutana mezani na kupeana zabuni.
Akizungumza baada ya kuzindua barabara na ujenzi wa Daraja Kwamela -Lukwambe, Chalinze mkoani Pwani, yenye urefu wa km.11
7 uliogharimu milioni 365.9 na upande wa daraja milioni 190.2, Mzava alieleza mfumo huo umetengenezwa ili kusaidia kila mzabuni.
"Tumefurahi sana kuona TARURA katika kutangaza zabuni mradi huu walipitisha kwenye mfumo huo"
"Mfumo huu mzabuni anaingia katika mfumo,anaomba zabuni na mfumo wenyewe unachakata nani mwenye sifa na nani hana sifa"
Mzava alifafanua,mfumo huo umeondoa malalamiko ,na tabia za watu kukutana mezani na kupeana zabuni.
"Zamani tulikuwa na mfumo wa TANREP na sasa tuna mfumo wa NEST na waheshimiwa wabunge wametutungia sheria nzuri ya kusimamia mambo hayo na ndio maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kupunguza malalamiko na kuweka udhibiti katika matumizi ya umma "alisema Mzava.
Pamoja na hayo alikemea matumizi ya madawa ya kulevya.
Mzava alieleza, asilimia 90 ya vitendo vya uharibifu wa mazingira vinasababishwa na shughuli za kibinadamu.
Alikemea tabia ya kuchoma misitu,mapori kwa visingizio ya kuwa wanaandaa mashamba ama kufukuza Wanyama wakali.
Aliomba jamii iendeleee kutunza mazingira,kupanda miti kwa ajili ya manufaa kwa vizazi vijavyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.