Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amekabidhi msaada wa vyakula, vinywaji, na vifaa vingine katika Kituo cha Karibu Nyumbani kilichopo Boko Timiza, Wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani. Msaada huu umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kama sehemu ya juhudi zake za kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya kwa kushirikiana na jamii mbalimbali nchini.
Mhe. Kunenge alikabidhi vifaa na mahitaji mbalimbali ikiwemo:Mchele Kilogramu 200, Unga wa Sembe Kilogramu 100, Sukari: Kilogramu 100, Sabuni za kuogea Mabox Mawili 2 Diapers Katoni 4, Taulo za kike Boksi 4 ,Mafuta ya kujipaka Dozeni 4.5, Sabuni ya unga: Mifuko 7, Mafuta ya kupikia: Lita 40, Mbuzi wa kuchinjwa: Wawili,
Maziwa ya Lactogen: Makopo 6, Vinywaji vya Sayona Tunda: Dozeni 10,Soda: Katoni 6,Viungo vya chakula
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mhe. Kunenge alisema, “Pokeeni zawadi hii kutoka kwa Bibi yenu, kwani Rais wetu amefanya tukio la kidini. Dini zetu zinatufundisha kusaidia watoto na kuwapenda. Kama maandiko yanavyosema, ‘Tuache watoto wadogo wakimbilie kwetu na tuwalee kwa mikono ya upendo.’”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Bi. Ester Abeid, alisema kuwa kituo kwa sasa kinalea watoto 29, wakiwemo wasichana 14 na wavulana 15, huku uwezo wa kituo ukiwa ni kulea watoto 40 wote wakiwa chini ya umri wa miaka minne.
Watoto wa kituo hicho walitoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada huo na kumwombea dua, wakimtakia afya njema, moyo wa upendo, na ustawi wa Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.