Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo leo Februari Mosi 2021 ameungana na Wananchi wa Wilaya ya Mafia kukipokea Kivuko kipya MV Kilindoni kitakachofanya safari zake kati ya Mafia na Nyamisati Wilayani Kibiti.
Akizungumza na Hadhara hiyo Ndikilo amesema anamwakilisha Waziri wa Ujenzi Dkt Leonard Shamuriho ambaye anamajukumu mengine, akisoma Hotuba ya Mhe Waziri Ndikilo amesema Kivuko hicho kimenunuliwa kwa gharama ya Shilingi Bilion 5.3 fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali, Ujenzi wa kivuko hicho umefanywa na Songoro Marine Transport Boatyard Ltd ya I Mwanza. Amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha Vivuko vyote vinakuwa vya Uhakika na Salama kwa matumizi.
Akitoa Salaam zake kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ndikilo amesema;
Anamshukuru Mhe Rais kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa mwaka 2015 wakati alipomtuma makamu wa Rais kuomba kura. "Asante Mhe Rais Bingwa wa kufufua mambo mazito yaliyoonekana kushindikana"
Amesema Kivuko hiki ni ukombozi Mkubwa kwa Wanachi Wanyonge." Siyo kila Mwanachi alikuwa na Uwezo wa kutumia usafiri wa Anga".
Ameongeza kuwa Wilaya ya Mafia inakwenda kufunguka zaidi kiuchumi, Shughuli za biashara zitaongezeka mauzo ya Nazi, Samaki na Korosho. Amesema Bidhaa zitapungua Bei, kama vile Vifaa vya Ujenzi na Mafuta ya Dizeli na Petroli.
Ndikilo amesema kupitia kivuko hicho wanatarajia uwekezaji Mkubwa Mafia kufanyika,ametoa wito kwa Wawekezaji ndani na Nje ya Nchi kuchangamkia Fursa za Uwekezaji ambazo tayari zimeaniashwa kwenye Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa huo mbao ulizinduliwa 2019.
Ndikilo ametoa wito kwa Wananchi kuchangamkia Fursa za kiuchumi za uwepo wa Kivuko hicho, ametaja Fursa hizo ni usambazaji wa Chakula ndani ya kivuko, Ajira za Mabaharia, huduma ya kufanya Usafi wa Kivuko, Shughuli za ubebaji Mizigo, Ulinzi n
Kivuko hicho kitakuwa na Uwezo wa kubeba Tan 100 sawa na abiria 200, Magari 10 na mzigo.
Aidha, ameitaka TEMESA kutoa Mwongozo Nauli na kubandika kwenye mbao za matangazo.
Ameeleza kuwa Kivuko cha mtu Binafsi kolichopo kitaendelea kufanya kazi kama kawaida,
Amewaeleza Wanachi ahadi ya CCM ya Ujenzi wa Kivuko kingine iliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi 2020-25.
"Tunatarajia ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo kitajengwa kivuko kingine kwa ajili ya Mafia"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.