Mkuu wa Mkoa Pwani , alhaj Abubakari Kunenge amewaasa wahitimu wa JKT Kuwa wazalendo wa Taifa lao pamoja na kuzingatia nidhamu, utii, uaminifu, uhodari kwa kuzingatia kiapo kinavyowataka.
Aidha amewataka vijana kuwa makini na teknolojia na kutumia ujuzi,elimu na mafunzo waliyoyapata vizuri kwa ajili ya kujenga Taifa na kuinua uchumi.
Kunenge alitoa Rai hiyo ,alipokwenda kufunga mafunzo ya JKT kwa mujibu ya oparesheni Jenerali Venance Mabeyo katika viwanja vya Ruvu JKT 832 .
Awali alipata wasaa wa kuzindua jengo la wodi ya wanaume na wanawake Ruvu JkT ,maabara ya kutotoleshea vifaranga vya samaki katika kambi ya Ruvu JKT.
Kunenge amepongeza uongozi mzima kwa ujasiliamali kwani wahitimu wanapata fursa ya kujifunza elimu, ujasiliamali na uzalendo.
Mafunzo hayo yalianza na Jumla ya vijana 3,342 Juni 2022, na kukaa kambini miezi mitatu ya mafunzo ,kati ya vijana hao 3,326 wamehitimu mafunzo yao vijana 16 hawakufanikiwa kuhitimu kwa sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu na wengine kutoroka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.