Muungano kwetu ni Tunu, tujivunie, tuulinde na tufanye kazi kwa bidii. Nchi nyingi zimetamani kuungana zimeshindwa "
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati akitoa salaam hizo Aprili 26, 2023 wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika Kimkoa Wilayani Mkuranga.
Kunenge ameeleza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni Umoja na mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza Uchumi. Ameeleza kikubwa katika Umoja ni kukuza Uchumi. Ameeongeza kuwa Muungano huo ni zao la vyama vyetu vya siasa ya TANU na ASP.
Aidha amesema kuwa ,kupitia wiki ya maadhimisho haya ya miaka 59 wakazi wa Mkoa wa Pwani wamejifunza kuwa waasisi wetu wa Muungano hakuwa wabinafsi waliweka maslah binafsi pembeni na kutaka Maendeleo.
Pia ameeleza shughuli Mbalimbali zimefanyika katika wiki hii ya Muungano ikiwemo Upandaji Miti, Usafi wa Mazingira, Kongamano la Muungano na Uzinduzi wa miradi ya Maendeleo.
Ameeleza Changamoto za Muungano zilizobaki ni chache na zinazidi kufanyiwa kazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.