Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amezindua Kliniki ya Ardhi katika Kata ya Vikindu, wilayani Mkuranga.
Kliniki hiyo ambayo imezinduliwa Sept 6 lengo lake ni kusaidia wananchi wa wilaya hiyo kutatuliwa migogoro mbalimbali ya ardhi inayowakabili.
Baada ya uzinduzi na kusikiliza baadhi ya malalamiko ya wananchi alitoa mwongozo wa utatuzi wa migogoro hiyo kwa kutoa maagizo kwa viongozi wa wilaya kutatua kwa umakini Ili wananchi wenye migogoro waweze kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.
Kunenge pia amewahimiza wananchi wa Kata ya Vikindu kutumia huduma za kliniki hiyo ili kurasimisha maeneo yao kwa kufuata taratibu.
"Jitokezeni kwa wingi katika kliniki hii ambayo watakuwepo wataalamu wa idara ya ardhi ili mpate haki ya kukaa kwenye maeneo rasmi," alisema Kunenge.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Hadija Nasri amesema kuwa baada ya uzinduzi huo, kambi ya wataalamu itakaa katika Kata ya Vikindu kwa siku nane, ili kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za ardhi zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.
Hadija pia amemuomba Mkuu wa Mkoa, Abubakar Kunenge, kuongeza idadi ya wataalamu wa ardhi, kwani waliopo kwa sasa hawakidhi mahitaji ya wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.