Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka Wakuu wa wilaya za mkoa huo kusimamia kikamilifu suala la lishe bora katika Wilaya Zao.
Mhandisi Ndikilo alitoa rai hiyo rai wakati akifungua kikao cha piili cha tathmini ya mkataba wa lishe kwa kipindi cha Januari-Juni, 2020 kilichofanyika Julai 16 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Mjini Kibaha.
Mhandisi Ndikilo aliwataka viongozi hao wa Wilaya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu lishe bora ikiwa ni pamoja na kuhamasiha watoto kupewa chakula wakiwa shuleni.
“Ndugu wajumbe tumeona tatizo la udumavu kitaifa ni asilimia 31 na sisi katika mkoa Wetu tuna asilimia 23 kutokana na hali hii wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya tunatakiwa kusisitiza lishe bora Kila mmoja katika eneo lake" alisema Mhandisi Ndikilo.
Akiweka msisitizo Mhandisi Ndikilo aliwaeleza viongozi hao kuwa baada ya agizo hilo anatarajia kupata matokeo chanya kwa Kila mmoja kusimamia katika eneo lake na kuhakikisha kuwa asilimi ya udumavu Mkoani Pwani inapungua ikiwa ni pamoja na kuondoa idadi ya watoto wenye udumavu.
“Hakkisheni kuwa mnawahamasisha wazazi wenye watoto shuleni wanachangia chakula ili watoto waweze kuepuka tatizo la udumavu kwa kukosa chakula” aliongeza Mhandisi Ndikilo.
Mkuu huyo wa Mkoa pia alitumia fursa hiyo kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa kuweza kuvuka malengo ya kiwango kilichowekwa cha viashiria vya
mkataba wa lishe ambapo amezitaka Halmashauri nyingine za Mkoa huo kuiga mfano wa halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.