Katibu Tawala Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Skauti Mkuu wa Tanzania Rashid Mchatta ameeleza kuwa maadhimisho ya siku ya albino Duniani kwa mwaka 2024 yamepangwa kufanyika Kibaha Mkoani Pwani.
Ameyasema hayo leo Machi 14, 2024 wakati akifungua kikao cha kwanza cha Kamati ya maadhimisho hayo kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi za Mkuu wa Mkoa huo na kushirikisha baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama cha watu wenye ualbino pamoja na wadau wengine mbalimbali.
Katika kikao hicho, Mchatta ameeleza kuwa jumuiya hiyo imefuata taratibu zote na kupata baraka za kufanya maadhimisho hayo mjini Kibaha.
"Chama cha watu wenye ualbino Tanzania waliwasiliana na Mhe. Mkuu wa Mkoa akaridhia, wakawasiliana na Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI na wote wakaridhia, hivyo tufanye maandalizi mazuri ili kufanikisha maadhimisho haya yaliyopo mbele yetu kuanzia tarehe 11 hadi 13 Mwezi Juni Mwaka huu," amesema Mchatta.
Nae Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Godson Mollel amesema maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila Mwaka yaliasisi hapa Tanzania na watu wenye ualbino watanzania mwaka 2006 kisha kuenea Duniani kote yakiwa na lengo kuu la kuendelea kwa watu wenye ualbino kuwa ni watu kama wengine ili kuondoa dhana potofu mbalimbali juu yao.
Wamefafanua kuwa katika maadhimisho hayo, kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwa ni pamoja na upimaji Saratani, elimu juu ya uchaguzi, msaada wa kisheria kwa wananchi, maonesho ya bidhaa kwa watu wenye ulemavu wa aina yoyote pamoja na michezo mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.