Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge amewataka Maafisa Biashara wa Mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Lindi na Mtwara kuhakikisha Jitihada za Mhe Rais za Kuvutia Wawekezaji zinafikiwa.
"Mhe Rais anavutia Wawekezaji na ameshasema nini kifanyike jinsi gani hayo yanatekelezeka Maafisa Biashara mnapaswa kufanya, Vinara wa Utekelezaji ni ninyi Maafisa Biashara tuone Uwepo wenu (Visibility). Lazima muelewe matarajio ya Nchi ili muyatimize.
Ameyasema hayo Juni 27 2022 wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea Uwezo Maafisa Biashara wa Mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Mtwara na Lindi.
Amewaeleza kuwa Serikali imeamua kuanzisha Idara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuongeza ufanisi wa Sekta hiyo.
Amewataka kuhakikisha wanatoa huduma Bora kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara
"Lazima tutoe huduma bora, lazima tujue wateja wetu ni Wafanyabiashara, huduma bora inabadilika mara kwa mara kwa Wafanyabiashara" Ameeleza Kunenge.
Amewaeleza kuwa Tanzania tupo eneo la Kimkakati Strategic position na kila Afisa Biashara anatakiwa kujua Fursa za Uwekezaji zilizopo kwenye Eneo lake.
Amewataka kusoma na kutumia Takwimu za Taasisi mbalimbali katika Kushauri na Kufanya Maamuzi "Wawekezaji wanapokuja manawapa Takwimu gani? Amehoji Kunenge-
"Wajibu wenu kuhakikisha Spidi ya Teknolojia mnakwenda nayo mkishindwa mtakuwa hamfai Maafisa Biashara mnatakiwa msome kila kitu" amesistiza Kunenge
Ameeleza kuwa utafiti unaonesha Maafisa Biashara wanatumika zaidi kama wakusanya Mapato badala ya kuwa wasaidizi na washauri wa Wafanyabiashara na Wawekezaji. Amewataka baada ya mafunzo hayo kubadilisha fikra na mitazamo yao na kuwa watoa huduma na msaada kwa Wafanyabiashara.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa Amewataka Maafisa Biashara hao kutokuwa maafisa Biashara wa Ofisini badala yake kuwasadia na Kushauri Wafanyabiashara. Aidha amekemea tabia ya baadhi ya Maafisa Biashara kufoji Leseni za Biashara kund B na kuwaeleza kuwa sasa wameandaa mfumo ambapo leseni zote zitatolewa kwa njia ya mtandao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.