Maagizo mbalimbali aliyotoa Rais JOHN POMBE MAGUFULI mkoani Pwani katika wilaya tatu za Mkuranga , Kibiti na Rufiji yametekelezwa na mengine yameshaanza kufanyiwa kazi.
Maagizo hayo ni pamoja na kutengezwa kwa gari la kubeba wagonjwa katika halmashauri ya wilaya ya Rufiji, kujengwa kwa vyoo vya stend ya mabasi ya Kibiti na Kutatua mgogoro wa Ardhi yenye ukubwa wa hekari 1,750 katika wilaya ya Mkuranga
Rais John Pombe Magufuli alitoa maagizo hayo tarehe 30 Julai baada kuzungumza na wananchi wilaya hizo ambao walimweleza kukabiliwa na kero mbalimbali , wakati akiwa njiani akitokea kijijini LUPASO wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwenye maziko ya aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Hayati Benjamini Mkapa.
Kufuatia Maagizo hayo mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis Evarist Ndikilo amekabidhi gari la kubebea wagonjwa la halmashauri ya wilaya ya Rufiji baada ya kufanyiwa matengezo
Kwa mujibu wa Mhandisi Ndikilo Maagizo mengine yameanza kufanyiwa kazi ambapo ujenzi wa vyoo vya stend katika wilaya ya Kibiti umeshaanza na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 8/2020 , huku mgogoro wa ardhi ukielezwa kushughulikiwa tarehe 4Julai 2020 na waziri wa ardhi ambaye anatarajia kufanya ziara katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kwenda kutatua mgogoro huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.