• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Madaktari Bingwa 64 wawasili Pwani kwa Huduma maalum chini Mpango wa Rais Dkt Samia

Posted on: June 9th, 2025

Timu ya madaktari bingwa 64 walioko chini ya mpango maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewasili mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa katika halmashauri zote za mkoa huo, pamoja na kubadilishana ujuzi wa kitaalamu na watumishi wa afya walioko katika vituo mbalimbali.

Mratibu wa timu hiyo kutoka Wizara ya Afya, Bw. Joachim Masunga, amesema kuwa ujio wa madaktari hao, ambao ni wa mara ya tatu mkoani humo, unalenga kupunguza changamoto zinazowakabili wakazi wa Pwani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupata huduma za kibingwa.“Kwa kuwaleta madaktari hawa karibu na wananchi, tunalenga kupunguza gharama na usumbufu wa usafiri wa wagonjwa pamoja na kuimarisha huduma za afya katika mkoa huu,” alisema Masunga.

Madaktari hao watakuwa mkoani Pwani kwa kipindi cha siku tano na wamesambazwa katika hospitali za halmashauri zote tisa za mkoa, ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa usawa na kwa wakati.

Akizungumza baada ya kuwapokea madaktari hao, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dkt. Kusirie Ukio, alisema kuwa ujio wa timu hiyo ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya na kupunguza idadi ya rufaa zinazotumwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukilazimika kuwapeleka wagonjwa Dar es Salaam kwa ajili ya huduma za kibingwa. Ujio wa madaktari hawa utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza rufaa hizo na kuleta unafuu kwa wagonjwa na familia zao,” alisema Dkt. Ukio.

Mpango huu ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha kuwa huduma bora za afya zinapatikana hadi ngazi ya msingi, na kwamba kila Mtanzania anapata huduma stahiki bila vikwazo vya kijiografia au kiuchumi.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Madaktari Bingwa 64 wawasili Pwani kwa Huduma maalum chini Mpango wa Rais Dkt Samia

    June 09, 2025
  • RC Pwani apokea msaada wa Ng’ombe 300 na Mbuzi 2,000 kwa Ajili ya Ibada ya Iddi kutoka Taasisi ya IDDef ya Uturuki.

    June 06, 2025
  • Mchatta Afungua Mashindano ya Umisseta Kimkoa

    June 07, 2025
  • Naibu Katibu Mkk OR- TAMISEMI azuru Mkoa Pwani kwa ukaguzi wa Huduma za Afya

    June 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.