Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Pwani wamemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kwakupewa ushirikiano na mazingira mazuri ya wao kuweza kutekeleza Miradi mbalimbali katika jamii wanazozisaidia.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Direct Aid Dr.Adam Othman wakati wakizindua mradi wa kituo Cha elimu Cha taasisi ya wasioona ya Waisalmu ya (VIMDAT) katika Kijiji Cha mwanambaya Mkuranga mkoani Pwani
Aidha Sheikh wa Mkoa Pwani alhaji khamisi Mtupa amezikumbusha mamlaka kuwatendea wema wenye Uhitaji nchini kupata tahfifu ya Mungu.
Awali akisoma Risala Mwl.Musa njechele ametaja Changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo Uhitaji wa Miundombinu ya Barabara Umeme na Maji.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe.Abubakar Kunenge kwa upande wake amezitaka Taasisi hizo kuwa licha ya kuwajengea miundombinu na kuwapa taaluma pia wawazeshe walemavu hao ili waweze kujiingizia kipato na kujitegemea
Akitoa shukrani rais wa Taasisi ya wasioona ya Waisalmu (VIMDAT) Salum Benedictor amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa Uongozi wake uliotukuka unao wajali watu walemavu pia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.