Machi 8, 2025, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, ameshiriki kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kisemvule, Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Subira Hamisi Mgalu, Mbunge Viti Maalum kutoka Mkoa wa Pwani.
Pamoja na mambo mengine, Subira alikiri juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi, jamii, siasa, kilimo na sekta nyingine, licha ya kuwa yeye ni mwanamke.
“Tunapoadhimisha siku hii, tunajivunia maendeleo makubwa katika sekta zote, na kinara wa haya yote ni Mwanamke ambaye ni Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Subira.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Mchatta, aliwapongeza wanawake kwa kuwa wao ni wazazi na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwaheshimu.
“Sisi kinababa tunawaheshimu kwa sababu mmetuzaa, Kwa hiyo, naomba tuendelee kuwaheshimu na kuwaombea dua wanawake” alisema Mchatta.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.