Katibu Tawala Mkoa Wa Pwani ,Rashid Mchatta amewaasa watumishi wa mkoa huo kufanya kazi kwa weledi ,kufuata miongozo ya utumishi wa umma ili kutimiza malengo ya kimaendeleo na kuinua uchumi wa mkoa.
Aidha amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wanafanikisha Malengo hayo.
Hayo ameyasema leo Machi 30 wakati wa makabadhiano ya Ofisi na aliyekuwa katibu Tawala Mkoa Pwani Zuwena Omary ambae amehamishiwa Mkoani Lindi.
Mchatta ameeleza kila mtumishi atimize wajibu wake kazini na kuwa waadilifu ili kumsaidia Mkuu wa Mkoa huo .
"Kila mtu afanye kazi yake kwa uadilifu wa hali ya juu ili tumsaidie mkuu wa Mkoa kufikia Malengo yake, inapaswa kwenda na kasi ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan pasipo kufanya kazi kwa mazoea "
Nae aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Zuwena Omary amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano Mchatta kama walivyokuwa wakimpa yeye na kupelekea kupiga hatua kwenye baadhi ya Malengo ya Mkoa.
"Binafsi nawashukuru sana watumishi wote wa Ofisi hii kwa ushirikiano mlionipa , ushirikiano ule mkauendeleze kwa Katibu Tawala Mchatta"
Akitoa neno la shukran kwa niaba ya watumishi wote Katibu Tawala Msaidizi Elimu Sara Mlaki amempongeza Katibu Tawala Zuwena kwa uhodari wake wa kazi aliounyesha wakati akiwa Mkoani Pwani.
Katibu Tawala Mchatta amehamia Mkoani Pwani March 2023 akitokea Mkoani Rukwa na aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Pwani Zuwena Omari Jiri amehamia mkoani Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.