Wakurugenzi nchini wametakiwa kuhakikisha hoja zote za mkaguzi wa hesabu za serikali CAG zitafutiwe majibu ili kuondoa hisia kuwa kuna ufisadi.
Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Wakurugenzi wa Miji, Manispaa na Majiji yaliyofanyika kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere.
Mchengerwa amesema kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kusikiliza kero za wananchi ili kutekeleza dhana ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo.
"Hapo hamkuchaguliwa kwa bahati mbaya bali ni imani aliyokuwa nayo Rais msiwe wanyonge na msishiriki vitendo vya rushwa na mnapaswa kumtanguliza Mungu kwani kuwatumikia wananchi ni ibaada,"amesema Mchengerwa.
Amewataka Wakurugenzi hao wasijikweze na wawe karibu na wananchi wajishushe wafanye kazi kwa weledi uadilifu na wasibweteke kwa kuteuliwa
"Hakikisheni mnakuwa na mahusiano mazuri na wananchi na nyie kwa nyie na watumishi na lazima wajue changamoto kwenye maeneo wanayo yasimamia na wasisubiri fedha za serikali wawashirikishe wadau na wananchi,"amesema Mchengerwa.
Amesema kuwa ukusanyaji mapato ni kipaumbele cha serikali kwani mapato yakiwa makubwa yatasaidia kutoa huduma kwa wananchi na kupeleka maendeleo kwani hilo Rais analisisitiza sana kwa maendeleo.
"Tumieni mifumo ya kieletroniki katika ukusanyaji wa mapato acheni matumizi ya fedha mbichi na kuepuka ukusanyaji wa mapato ambao hautumii mashine kwani unasababisha mapato kupotea na kuwaondoa baadhi ya watumishi wanaosababisha upotevu wa mapato na kukusanya nje ya mfumo na fedha zilizo nje zirejeshwe,"amesema Mchengerwa.
Aidha kuchukuliwa hatua kwa watumishi wasio waaminifu wasisubiri hadi waziri achukue hatua kwani wakiharibu wao ndiyo watakaowajibishwa na wawe wabunifu na wawape mafunzo maofisa biashara wasikae maofisini na waongeze vyanzo vya mapato.
Naye Annastazia Tutuba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manyoni amesema kuwa mafunzo hayo wamewakumbusha kutekeleza majukumu yao na moja ni kukondokana na hati chafu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe Mwashaban Mrope amesema kuwa watasimamia fedha nyingi ambazo zimetolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.