Mkuu wa Mkoa wa Mkoa Mhe Abubakari kunenge amezindua mpango wa mfumo wa m.mama Mkoani humo , ukumbi wa wauguzi Kibaha Mjini,mfumo ambao utarahisisha masuala ya usafiri wa dharura ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Akizindua Mpango huo June 15 ,Kunenge amesema mkoa wa Pwani Vifo vya wamama wajawazito vimepungua kwa asilimia 46.6, kutoka vifo 96 kwa mwaka 2018 kati ya akinamama waliofika vituoni 43,488 hadi kufikia vifo 35 kwa mwaka 2022 kati ya akinamama 56,439.
Aidha Vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa asilimia 5.5 kutoka 475 kwa mwaka 2018 na kufikia vifo 390 kwa mwaka 2022.
Ameeleza licha ya mafanikio na changamoto zilizopo, ujio wa mfumo wa m.mama utaleta matokeo chanya katika kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Ameongezea kuwa kila mmoja kwa nafasi yake akatimize wajibu wake, ili kutekeleza mfumo huo.
Awali mganga mkuu wa mkoa wa Pwani dkt.Gunini Kamba anaeleza, changamoto kubwa ni jiografia magari ya wagonjwa kutofika kwa wakati mama akipata dharura lakini m.mama itakuwa mkombozi.