Mwenge wa Uhuru utapitia miradi 28 yenye thamani ya trilioni 8.5 wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambapo umekagua mradi mkubwa wa
Kongani ya Viwanda ya SINOTAN, Kata ya Kwala ambao hadi kukamilika utagharimu trilioni 8.4.
Aidha umeweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara kutoka barabara ya Morogoro kwenda ofisi za Halmashauri, yenye urefu wa mita 300 kiwango cha lami, thamani mil490,018,125 fedha za ujenzi kutoka Serikali Kuu -Maendelo ya Jimbo.
Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava, Meneja wa TARURA wilayani Kibaha , Samwel Ndoveni alisema,
mradi umetekelezwa na Mkandarasi M/S Globalink General Contractors Ltd.
Nae Mzava ameridhishwa na mradi huo wa barabara,na kusisitiza umuhimu wa manunuzi ya umma kutumia mfumo wa kidigital wa manunuzi ya umma Nest ambao unasimamiwa na mamlaka ya udhibiti ya manunuzi ya umma (PPRA).
Mzava alifafanua,mfumo huo umeondoa malalamiko ,na tabia za watu kukutana mezani na kupeana zabuni.
Katika hatua nyingine, Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la uzinduzi wa mradi wa maji kijiji cha Ruvu Stesheni, kumtua mama ndoo kichwani,mradi ambao unasimamiwa na Mamlaka ya maji safi Na mazingira Vijijini (RUWASA) .
Chanzo cha mradi huo ni kisima chenye uwezo wa kutoa lita 11,820 kwa saa na kina urefu wa mita 43, gharama za mradi mil328,719,109.94 kupitia mfuko wa Taifa wa maji (NWF).
Mwenge huo pia umekagua na kufungua mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu matano ya vyoo shule ya msingi Kilangalanga na kituo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Mlandizi.
Awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Bagamoyo, Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Nikkison John alisema, Mwenge huo utapitia miradi 28 katika halmashauri ya Kibaha Mjini na Kibaha Vijijini ,yenye thamani ya trilioni 8.5.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.