• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Mkoa wa Pwani Waendelea Kung’ara katika Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).

Posted on: September 30th, 2025

Mkoa wa Pwani umeendelea kuwa mfano wa mafanikio katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kupunguza umasikini uliokithiri na kuboresha maisha ya wananchi wa kipato cha chini.

Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia uchumi na uzalishaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Shangwe Twamala, aliwaasa waratibu wa mpango huo kuhakikisha kuwa vikundi vilivyoundwa na kunufaika na TASAF awamu ya pili vinasimamiwa ipasavyo.

Aidha alihimiza wapewe elimu, mitaji na fursa kupitia mikopo ya asilimia 10 kutoka mapato ya Halmashauri, ili kuwawezesha kusimama kiuchumi na kuepuka kurejea katika hali ya umasikini.

Twamala alitoa wito huo leo, Septemba 30,2025 wakati akifungua kikao kazi cha mwaka cha Utekelezaji wa Mpango wa TASAF III Awamu ya Pili, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kibaha.

Aliishukuru Serikali kwa kutoa zaidi ya sh bilioni 44 kwa ajili ya kuendesha na kuwezesha miradi mbalimbali chini ya mpango huo.

Alisema mpango huo umeleta manufaa makubwa kwa familia zenye hali ngumu za kiuchumi, hasa kwa kuboresha huduma za jamii na kuinua vipato vya kaya.

Kwa mujibu wa Shangwe ni muhimu miradi yote inayotekelezwa kukamilika kwa wakati ili iweze kuwanufaisha walengwa na kuendana na dhamira ya serikali ya kuwainua wananchi.

Kwa upande wake, Mhandisi Abel Bimbiga, Mwakilishi kutoka Makao Makuu ya TASAF, aliupongeza mkoa wa Pwani kwa kuwa miongoni mwa mikoa inayotekeleza mpango huo kwa mafanikio makubwa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo, Mratibu wa TASAF Mkoa wa Pwani, Roseline Kimaro, alieleza Mkoa wa Pwani ulikuwa miongoni mwa maeneo ya kwanza kufanya majaribio ya awali ya mpango huo, ambapo Wilaya za Bagamoyo na Kibaha ziliteuliwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza.

Kimaro alisema ,mkoa umetekeleza miradi mbalimbali ya afya na elimu katika maeneo 16, ikiwemo jengo la mochwari katika Hospitali ya Wilaya ya Msoga, wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya Miono, Chalinze, Zahanati ya Mwanalugali, Nyumba za watumishi katika Zahanati ya Vikawe wilayani Kibaha, Majengo matano katika Kituo cha Afya Nyamatanga wilaya ya Kibiti na Bweni la wasichana na nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari Samia wilayani Rufiji.

Kufuatia mafanikio ya awali, serikali ilipanua TASAF hadi kufikia wilaya zote nchini na mikoa yote 26 ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na juhudi za kupunguza umasikini.

Kimaro anasema hadi kufikia Juni 2025, Mkoa wa Pwani ulikuwa umeunda jumla ya vikundi 1,601 vya wanufaika, vyenye wanachama 16,495, kati yao, 14,568 ni wanawake na 1,927 ni wanaume, kupitia vikundi hivyo, wanufaika wameanzisha miradi ya kiuchumi, kuweka akiba na kujiimarisha kiuchumi.

"Wanufaika wamepata mafanikio makubwa katika huduma za msingi kama vile elimu, afya, lishe, makazi bora, na shughuli za kilimo, ufugaji, biashara ndogondogo, usindikaji wa bidhaa, ushonaji na ufumaji.

Kimaro alibainisha kuwa jumla ya mtaji wa vikundi hivyo umefikia sh milioni 330 hadi sasa.

"Lengo la serikali kupitia TASAF, si kutoa msaada wa muda mfupi pekee, bali ni kuwawezesha walengwa kuwa na msingi madhubuti wa kiuchumi na kuweza kujitegemea hata baada ya mpango kumalizika.

Anaeleza mafanikio haya ni matokeo ya ushirikiano wa karibu kati ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, viongozi wa jamii na wanufaika wenyewe, na kueleza matumaini kuwa mpango huo utaendelea kubadilisha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo endelevu ya Mkoa wa Pwani na taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Kunenge: Aagiza Mradi wa IPOSA ulete Matokeo yanayoonekana.

    October 02, 2025
  • Mkoa wa Pwani Waendelea Kung’ara katika Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).

    September 30, 2025
  • Rais Samia Aipongeza Pwani Kwa Kuibeba Vyema Ajenda ya Kitaifa ya Uwekezaji Katika Viwanda.

    September 28, 2025
  • Serikali Yatoa Bilioni 19.8 Kujenga Soko la Kisasa na Barabara Mbili Kibaha.

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.