Leo Septemba 25, 2025, Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa wa Pwani Grace Tete amefungua rasmi kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwa kipindi cha Januari–Juni 2025.
Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta za serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi wa dini, waandishi wa habari na watoa huduma kutoka ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kuangalia mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8.
“Serikali ya Awamu ya Sita inatambua kuwa miaka ya awali ya mtoto ni muhimu sana katika ukuaji na maendeleo ya rasilimali watu. Ni lazima tuwekeze kwenye afya, lishe, elimu ya awali, malezi yenye mwitikio na ulinzi wa mtoto,” alisema Tete.
Programu hii ni sehemu ya juhudi za serikali na wadau katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya msingi ya kuishi, kukua na kujifunza katika mazingira salama na yenye tija.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.