Mkurugenzi Mtendaji wa “Global Fund” Peter Sand leo Septemba 7, 2022 ametembelea Mkoa wa Pwani na kukagua utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko huo ambayo ni kuzuia maambukizi ya na Ukimwi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto - PMTCT, Malaria na Kifua Kikuu - TB ya amesema Mfuko huo.
Katika ziara yake hiyo Sand aliongozana na Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu na kupokelewa na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge aliyeongoza msafara wao hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Zahanati ya Disunyala halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Zahanati ya Mwendapole Halmashauri ya Kibaha mji ambako baada ya kukagua shughuli hizo, Mkurugenzi Sand alieleza kuridhishwa na huduma zinazotolewa hususani kukabiliana na maambukizi ya ukimwi, malaria, kifua kikuu lakini pia akaeleza kuwapo ubora katika utoaji huduma za mama na mtoto.
Sand aliwahikikishia wanachi kuwa Mfuko huo utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza mapambano dhidi magonjwa hayo.
Katika ziara hiyoq, wakiwa Katika Zahanati ya Disunyala na kuzungumza na wananchi, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alielekeza matibabu ya malaria kutolewa bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali nchini na akaelekeza watoa huduma kuacha kutoza fedha kwa wananchi wanaofika kufanya vipimo vya malaria na kifua kikuu na akasema "Kipimo cha malaria cha haraka ni (MRDT), dawa za malaria ALU na sindano ya malaria kali ni bure, pia kipimo cha kifua kikuu nacho ni bure kwasababu “Global Fund” wanatusaidia tuweze kutokomeza magonjwa haya matatu.”
Waziri Ummy pia aliwataka wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kutoacha kutumia dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo (ARV) na pia kusitisha ngono zembe kutokana na kasi ya maambukizi iliyopo Kwa sasa ambapo alisema kuwa kumekuwepo na kusua sua kwa matumizi ya dawa hizo kwa baadhi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi jambo ambalo ni la hatari.
“Kati watu 100 wanaoishi na virusi vya ukimwi hapa Tanzania, ni 95 ndio wanaotumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI, tumeiona hiyo hali ya kusuasua kwa matumizi ya ARV,” alisema Waziri Ummy na akaongeza kuwa Wakati watanzania wakikaribia kuushinda UKIMWI ndiyo watu wanaanza kurudi nyuma hivyo akasisitiza waathirika kutoacha kutumia dawa hizo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema Global Fund ndio wanaosaidia maboresho yanayosaidia kuondokana na changamoto za kiafya na kwamba wanasaidiana na Serikali ya Rais Samia Suluh Hassan katika kuboresha huduma hizo.
Kunenge aliishukuru Serikali kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anafika na kutembelea na kujionea baadhi shughuli na huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo Mkoani Pwani ambazo zinatokana na ufadhili wa mfuko huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.