• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI AFANYA ZIARA MKOANI PWANI

Posted on: November 29th, 2017

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)Simon Sirro amewahakikishia wananchi Mkoani Pwani kuwa silaha zote zilizochukuliwa na wahalifu wa  huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote mkononi mwa dola na kusambaratisha mtandao wa kiuhalifu .

Aidha ametoa rai kwa wazazi na walimu kutoa taarifa kwenye vituo vya polisi mara watakapobaini kuna mwanafunzi mtoro ama hajaripoti shule kwa miezi kadhaa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.

Pamoja na hayo IGP Sirro, amesema vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinashirikiana na nchi ya Msumbiji kupambana na wahalifu waliobainika kukimbilia nchini  humo wakitokea Tanzania.

Aliyasema hayo wilayani Kibaha, Mkoani Pwani, katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo pia alizungumza na viongozi wa mashirika ya umma,wazee maarufu ,wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama ya  Mkoa wa Pwani.

IGP Sirro alieleza kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kupambana na yeyote atakaekuja kwa moto wataenda nae kwa moto na atakaekuja baridi wataenda nae baridi.

Alisema Serikali imeshinda kwa hilo na hali kwa sasa ni shwari katika wilaya hizo. IGP Sirro alieleza amepatiwa taarifa ya wanafunzi zaidi ya 1,300 Mkoani Pwani kuwa ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi washirikiane kusaidia Jeshi la Polisi kujua walipo.

“Kuna baadhi misikiti, makanisa yanadaiwa yanayotumia watoto hawa katika masuala ya kiuhalifu hivyo kuna kila sababu ya kuingia ndani kutafuta suluhu”

“Ni kazi yetu wazazi jamii na walimu kushirikiana, na hapa ni muhimu wazazi wasaidie kusema watoto wao walipo ili kuwa na usalama” alisema .

Katika hatua nyingine IGP Sirro alielezea kuwa, viongozi wa dini wana nafasi ya kuhakikisha wanatumia eneo lao kuhubiri amani. “Tusidharau taarifa hata kama ni ndogo, tusibweteke, umoja ni nguvu, tusaidiane kukomesha vitendo vya uvunjifu wa amani ” alifafanua IGP Sirro.

Akizungumzia changamoto ya wahamiaji haramu alisema, wanashirikiana na uhamiaji kuusaka mtandao unaohusika kufanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu. IGP Sirro alisema hawatamvumilia yeyote anaekumbatia wahamiaji haramu kwani ni chanzo cha kusababisha kuleta magaidi  na kusafirisha bidhaa za haramu. Alisema kwasasa wamejipanga kutaifisha mali za wafanyabiashara hao wa wahamiaji haramu na usafiri unaotumika kuwasafirisha.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo ameshukuru kuwepo kwa kanda maalum ya Rufiji kwani imeweza kuleta mafanikio makubwa. Alisema kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya sintofahamu,watu walisitisha shughuli zao za maendeleo, biashara zilikwama,watu na baadhi ya viongozi walihama nyumba zao na wengine kulala saa 12 jioni kwa kuhofia mauaji.

Mhandisi Ndikilo alieleza sasa Kibiti na Rufiji hali ni shwari kutokana na kuimarishwa kwa ulinzi.

Aliwataka pia wawekezaji na wadau mbalimbali Mkoani Pwani, kujitokeza kushirikiana ili kusaidia kutatua changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ,usafiri na kujenga Vituo vya Polisi.

Mhandisi Ndikilo, alisema kuwa Mkoa wa Pwani umesheheni viwanda vya kutosha hivyo ni vyema kusaidia mambo hayo kwa manufaa ya wote.

“Tukikumbwa na uhalifu tunapigia simu polisi, tusiwe wa kwanza kulaumu wakati wa matatizo, tukumbuke kuwasaidia ili kufanikisha kazi zao kiufanisi” alisema Mkuu wa Mkoa .

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, ACP Jonathan Shanna alisema ziara hiyo ni neema kwao na wamepewa maagizo mbalimbali ambayo watayafanyia kazi.

Kamanda Shanna alisema wamemfikishia kero IGP zinazowagusa Askari Polisi ikiwemo upungufu wa makazi .

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.