• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Afanya Ziara Kiwandani Bagamoyo, Apongeza Uwekezaji na Ushirikishwaji wa Vijana katika Uundaji wa Magari ya FAW.

Posted on: July 25th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge,  amefanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha kuunganisha magari  aina ya FAW cha Kampuni ya Rostar Vehicle Equipment Limited kilichopo wilayani Bagamoyo, ambapo  alipata fursa ya kukagua Ujenzi wa kiwanda na kujionea magari mbalimbali yaliyokwisha kuunganishwa, hususan ya aina ya Tipper na kupokea taarifa ya Mradi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kunenge alieleza kuridhishwa kwake na namna wawekezaji wa kiwanda hicho walivyoshirikisha vijana wa Kitanzania katika shughuli za uundaji wa magari, akisisitiza kuwa vijana hao wana uwezo mkubwa na ubunifu wa hali ya juu.

“Vijana wapo na wana uwezo mkubwa wa kufanya shughuli hizi. Ni wafanyakazi wabunifu na wenye juhudi. Nawapongeza sana,” alisema Mhe. Kunenge.

Aidha, aliwashukuru wawekezaji kwa kuamua kuwekeza wilayani Bagamoyo na kusisitiza kuwa uwekezaji huo ni mkubwa na muhimu kwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

“Hiki ni kiwanda kikubwa cha kuunganisha magari ya FAW barani Afrika, nawapongeza sana kwa maono haya makubwa,” aliongeza Kunenge.

Pia aliwapongeza kwa kuwa waaminifu katika ulipaji wa kodi, jambo alilosema linaonesha uzalendo na uelewa wa wajibu wao kwa taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Bai Xinguo, alisema ujenzi wa kiwanda hicho ulianza mwezi Juni 2024 na sasa umekamilika kwa awamu ya kwanza  ambapo tayari kimeanza uzalishaji wa magari. Kiwanda hicho kinategemea kuzalisha magari, trailer za magari,  tank, Pamoja na cranes

Bw. Xinguo alieleza kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha magari 500,000 kwa mwaka na tayari wamepokea oda ya magari 1000 kutoka kwa wateja mbalimbali.

Aidha, alitoa shukrani kwa serikali kwa usaidizi katika hatua mbalimbali za kuanzisha kiwanda hicho, huku akiomba msaada zaidi katika ujenzi wa barabara ya kufika kiwandani hapo.

Katika kujibu ombi hilo, Mhe. Kunenge aliahidi kuwa serikali ya mkoa italifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka husika ili kuhakikisha miundombinu ya kufika kiwandani inaboreshwa.

Katika hatua nyingine Mhe Kunenge amemuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuanza kupanga Mji eneo Hilo na watu wote wanaomiliki Ardhi eneo Hilo wafuate ramani ya mipango miji.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mkuu wa Mkoa wa Pwani Afanya Ziara Kiwandani Bagamoyo, Apongeza Uwekezaji na Ushirikishwaji wa Vijana katika Uundaji wa Magari ya FAW.

    July 25, 2025
  • Rais Samia kuzindua Bandari Kavu ya Kwala na miradi mikubwa ya miundombinu Mkoani Pwani.

    July 22, 2025
  • Pwani Yazindua Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Bure Zaidi ya 971,000 kwa Vita Dhidi ya Malaria.

    July 18, 2025
  • Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Aongoza Ufunguzi wa Kikao cha Mpango wa MTAKUWWA II.

    July 18, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.