Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist W. Ndikilo amewataka wananchi wa Kisarawe kufufua zao la korosho kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo Wilaya hiyo ilikuwa ikisifika kwa kulima zao hilo.
Hayo aliyasema wakati akiongea katika mkutano wa wananchi uliofanyika katika kata ya Mzenga wakati alipofanya ziara yake ya kuhamasisha kilimo cha mazao ya chakula na biashaara Wilayani hapo.
Aidha Mhandisi Ndikillo alieleza kwamba zao la korosho liwe azimio la baraza la Madiwani Wilayani humo kwani kulima korosho kwa wingi kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini kwa wananchi wa Kisarawe.
Mhe. Ndikillo pia ameonya wizi unaofanywa na baadhi ya vyama vya Ushirika vya Msingi vya Korosho(AMCOS) kwa wanunuzi wa korosho pia amewapiga marufuku kangomba kwani inasababisha hasara kwa wakulima wa korosho badala yake utumike mfumo wa stakabadhi ghalani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.