...Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Evarist W. Ndikilo amewapongeza na kuwashukuru watu wa Marekani kwa ufadhili wa miradi mbalimbali wanaofanya nchini.
Mhe. Ndikilo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa utambulisho wa Mradi mpya wa Kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa makundi maalum na yaliyo katika hatari ya maambukizi katika jamii.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Shirika la ICAP Mkoa wa Pwani wakati alipokuwa akielezea jinsi Mradi wa Kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI(VVU) utakavyotekelezwa Mkoani Pwani
Mradi huo wa miaka mitano (5) unafadhiliwa na watu wa Marekani kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Ukimwi (PHEPA), utatekelezwa katika Mkoa wa Pwani na Shirika la ICAP ambapo kwa kuanzia utaanza kutekelezwa katika Halmashauri za Kibaha Mji, Bagamoyo na Mkuranga. Baadae mradi utafanya shughuli zake katika Halmashauri za Wilaya ya Kibaha na Rufiji.
Aidha, Mhe. Ndikilo amesema kuwa mradi huo utasaidia sana katika jitihada za Mkoa na Wizara kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa ujumla. Hivyo amewataka wadau wote walioshiriki katika mkutano huo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.